Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya HABARI ZA MASTAA

SUAREZ ATANGAZA KUACHANA NA MADRID

Picha
Madrid, HISPANIA. Klabu ya Athletic Madrid imetangaza kuachana na mshambuliaji wake hatari Luis Suarez (35) baada ya msimu huu kuisha. Suarez ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu ,yeye pamoja na Hector Herrera wataondoka klabuni hapo na kupewa heshima zote za kuagwa na mashabiki katika uwanja wa  Wanda Metropolitan. Katika msimu wake wa kwanza na Athletic Madrid amefanikiwa kuchukua kombe la LaLiga na kufumania nyavu mara 21 katika mechi za LaLiga huku msimu huu tayari ashaweka kimyani magoli 11.

KOFFI OLOMIDE AKUBALI UJIO WA WENGE

Picha
Kinshasa DRC Mwanamziki mkongwe barani Afrika Charles Antonio Mumba Olomide amefurahishwa na hatua ya wanamziki waliounda kundi la  WENGE MUSICA au WENGE MUSICA BCBG kuamua kuungana upya katika hatua ya kufufua kundi hilo.Kundi la WENGE MUSICA lilianzishwa na Didier Msika mwaka 1981 likipitia tena kwenye mikono ya JB MPIANA mnamo mwaka 1986 kablà ya kuvunjika mwaka 1997 huku sababu ikitajwa viongozi wake wakuu kutoelewana. Nguli huyu wa miondoko ya Sokous na Rhumba amesema anapenda kundi hili lirudi upya huku akizungumzia kile ambacho huwa kinatajwa kwamba yeye na Papa Wemba ndio walikuwa watu waliosababisha kundi hilo kufa amesema nafurahi sana WENGE MUSICA kurudi lakini mimi nilisemwa kuliua kundi hili lakini hiyo ilikuwa vita ya ushindani Wa kimziki na kutafuta ufalme pia wa mziki .

HISTORIA YA MAISHA YA PAPA WEMBA

Picha
Mwanamziki Papa Wemba alizaliwa 14 Juni 1949 na kufariki 24 April 2016,alizaliwa Lubefu Zaire ya Zamani. Papa Wemba ni mwamba Wa Mziki Wa Sukus na anafahamika Dunia kwa mtindo wake Wa uvaaji na utanashati ujulikanao kwa lugha ya Kifaransa yaani la Saperé. Umaarufu zaidi Wa Papa Wemba ulitokana na kundi lake la mziki la Viva la Musica  Mwaka 1969,Papa Wemba akiwa na hakina Nyoko Longo,Bimi Ombale,Moloko Leilei na Vuela Somo walikuwa vijana wa mwanzo watanashati na walijiunga na kuanzisha kundi la mziki la Zaiko Langa langa lililokuwa likiimba mziki Wa Sukusi.Tofauti ya mziki wa Sukusi na Rhumba la wakati huo wa makundi ya TP OK Jazz au Afriza International  ni kwamba mziki huu unaenda kasi mno.Mziki huu ulianzishwa na vijana waliochoshwa na mziki wa Rhumba wa kukumbatiana mwanzo mwisho bila jasho ,wao walitaka toka nukta ya kwanza ya kuanza mziki ni kucheza mwanzo mwisho. Sukusi  ni kizazi cha nne cha mziki wa Rhumba kutoka Zaire,utamaduni waliopitia vizazi vinne na kuunda kile kizazi k

MOZEY BROWN - AGGY (Official Music Video)

Picha
 

MOZEY BROWN AACHIA WIMBO WAKE"MAMA LAO"

Picha
Dar es salaam. Msanii wa kizazi kipya Moses Joseph ameachia wimbo wake mpya ujulikanao kama MAMA LAO ambao kwasasa unapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, Audiomack,Boomplay,na Facebook. Meneja wa msanii huyo Mujuni Henry ,amethibitisha hilo rasmi kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku pia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Mpaka sasa wimbo huo unaendelea kufanya vizuri huku pia mashabiki wa mziki wa bongo fleva wakikiri kuwa msanii MOZEY BROWN anafuata nyayo za wasanii wa muda mrefu kwenye kiwanda cha mziki wa Tanzania yaani Bongo Fleva. MOZEY BROWN ni nani? Ni msanii wa mzazi kipya ambaye kwa sasa ameingia kwenye mziki kwa mara ya kwanza na akiwa ametoa wimbo wake huo mmoja wa " MAMA LAO" . Ni mkaazi wa jiji la biashara la Dar es salaam akiwa chini ya management ya mfanyabiashara MUJUNI HENRY.

DIAMOND NA ZUCHU WAPATA PIGO

Picha
Dar es salaam. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imezuia wimbo wa Diamond ft Zuchu ujulikanao kama "mtasubiri" kwa muda kutokana na kipande cha video kuonekana na tafsiri mbaya. Katika taarifa ya mamlaka hiyo nchini imeeleza video ya wimbo huo ina kipande kinachoonyesha Zuchu ni mwana kwaya ambaye yuko kanisani anaimba na ghafla anapigiwa simu na kupokea simu wakati anaimba kwenye kwaya. Kutokana na kitendo hicho kipande, hali imekuwa ya sintofahamu kwa waumini wa dini ya Ukiristo ambao wametafsiri kama udhalilishaji. Aidha,mamlaka imemtaka mmiliki wa wimbo huo Diamond kurekebisha maudhui ya video hiyo na pia kuomba watu na vyombo vya habari kutosambaza video hiyo.

DIAMOND NA ALIKIBA MAMBO SAFI

Picha
Dar es salaam. Msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz akipiga stori kwenye kipindi cha "THE SWITCH" cha radio WASAFI FM inayorusha matangazo yake kutokea Mbezi beach ,Dar es salaam. Diamond Platinumz amesema hana wasiwasi wa kufanya kolabo na msanii Alikiba na hana ugomvi nae isipokuwa ni maneno ya mashabiki ,wanaowashindanisha kwenye mziki. Akipiga stori ,alijibu baadhi ya maswali ya watangazaji wa redio hiyo waliotaka kufahamu kama ana bifu na msanii mwenzake Alikiba,Diamond alikataa akidai kwamba kumshindanisha na wasanii wa ndani ni kuikosea tasnia ya mziki wa Bongo Fleva na watanzania pia.Diamond ambaye alifika kutambulisha EP yake ya "FOA" kwa mashabiki wake amejitambulisha kuwa sasa ni msanii namba 3 kwa Afrika. ila kuna mawazo ambayo watanzania tunatakiwa tuyafute ,ili wewe uonekane mkubwa lazima ugombane na mtu,Mimi sina noma halafu kila mtu namuheshimu kwa upande wake" Diamond Platinumz kwasasa anatoka na EP ya FOA yenye nyimbo kama Fresh📝📣so

MAKONDA AMUITA GSM TAPELI

Picha
Dodoma. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Shaka Hamdu,leo machi 12,2022 amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Katibu huyo alitaka kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokaa hivi karibuni. Shaka ameeleza kati ya mambo yaliyojadiliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM,Taifa ni pamoja na kuchunguza vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi hasa kuwaonea raia kwa kuwabambikizia kesi. Baada ya taarifa h iyo,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda aliibuka na kuandika haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram "naunga hoja mkono ya kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ,wanalipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu.Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano. Haya ya Makonda yanajiri hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro wa nyumba yake iliyopo Masaki Dar es salaam inayothibitiwa na mfanyabiashara

TYSON FURY AMPA TANO KLITSCHKO

Picha
Marekani. Staa wa uzito wa juu duniani, Tyson Fury, amewaunga mkono mabondia wa Ukraine , Wladimir Klitschko na Vital Klitschko kwa kitendo cha kujitoa kuipambania nchi yao katika vita inayoendelea dhidi ya Urusi. staa huyo alisema"

HARMONIZE AZIDI KUONYESHA JEURI YA PESA

Picha
Msanii wa Bongo Fleva Harmonize akigawa hela kwa miongoni mwa mashabiki aliehudhuria kwenye tamasha lake  

SAT-B msanii kutoka BURUNDI akisherehesha

Picha
Dar es salaam. Msanii kutokea Burundi SAT-B naye ni miongoni mwa wasanii waliosherehesha kwenye "KONDE GANG CARNIVAL FESTIVAL".  

DRAKE ANUNUA NYUMBA YA NDOTO YAKE

Picha
Los Angeles. Rappa Drake wa nchini Marekani amenunua nyumba yenye thamani ya dola za marekani milioni 85 sawa na bilioni 187 za shilingi ya Tanzania. Nyumba hiyo iliyopo eneo la Beverly Hills mjini Los Angels nchini Marekani ina ukubwa wa futi za mraba 25,000 . Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala 10,bafu za kuogea 22,gereji za magari 11,gym na viwanja vya mchezo wa tenisi.

Harmonize FT Bruce Melodie-TOTALLY CRAZY (Official Video)

Picha
 Msanii wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya KONDE GANG,Harmonize ametoa video ya wimbo wake aliomshirikisha Bruce Melodies hujulikanao kama "Totally Crazy). __ TAZAMA VIDEO

IRENE UWOYA ATOA SIRI YA KULA BATA

Picha
Dar es salaam. Mrembo Irene Uwoya amesema hafahamu ni kiasi gani cha pesa huwa anatumia kula bata? Mrembwende huyo akipiga stori Ijumaa hii amesema watu wanakuwa wanafatilia mtindo wa maisha yake ya kula bata. Mrembo huyu wa tasnia ya filamu Tanzania Bongo movie ametoa siri ya kula bata na kundi kubwa la watu anaosafiri nao nje na ndani ya nchi kwa kusema" pesa haitafutwi bali inategwa". Irene Uwoya ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akitrend mitandaoni akila bata na watu wake pia na manunuzi ya magari ya thamani kubwa na matukio mbalimbali zikiwepo kumbukizi za kuzaliwa za watu wake wa karibu.

Gigy Money-SASAMBUA (AUDIO official)

Picha
 

Nay wa Mitego-Tumerogwa (Audio Official)

Picha
 

JUX ft GYAKIE - I LOVE YOU (Official video)

Picha
 

PAUL MAKONDA AZIDI KUPETA

Picha
Dar es salaam. Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ,Goodchance Reginald amesema mteja wake hakuwa amepewa wito wa kufika mahakamani zaidi ya kuziona habari hizo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Wakili Reginald ameyasema hayo leo katika mahakama ya Kinondoni jijini Dar es salaam na kuomba mahakama impe muda zaidi mteja wake ili kuwakilisha hati kinzani dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na mwandishi wa habari ,    Saed Kubenea ya kutaka kibali cha kumfutia kesi ya jinai. Kufuatia maombi hayo ,Hakimu mkazi Aron Lyamuya anayesikiliza shauri hilo ,amesema mahakama hiyo inampa Makonda siku 21 kuwasilisha hati hizo kinzani dhidi ya maombi ya kumfutia kesi ya jinai yaliyowasilishwa na Kubenea.

MDOGO WAKE DIAMOND AMKATAA RAYVANNY

 

MAMBO YA KUTISHA YA MFALME ZUMARIDI WA MWANZA

 Tazama mwanzo mwisho alichofanya Mfalme Zumri kwa huyu kijana.