JINSI YA KUJIPATIA HELA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

BIASHARA. Mtandao wa kijamii wa Facebook ni mmoja ya mitandao mikubwa ya kijamii duniani ukiwa na takribani watumiaji bilioni 4. Mtandao huu unaomilikiwa na kampuni ya META iliopo chini ya bilionea kijana Mark Zuckerberg. Mtandao huu ni miongoni mwa mitandao ya kampuni hii ya META ambayo pia inamiliki Whatsapp , Instagram na Messenger. NAMNA YA KUTENGENEZA PESA FACEBOOK Facebook kama ulivyo mtandao wa kibiashara huwa unatoa fursa ya watumiaji wake kunufaika na mtandao huu. Hili utengeneze pesa kwanza fungua 1) Facebook page: Eneo hili upatikana kwenye kushoto mwa ukurasa wa facebook. -Baada ya kufungua page ,vutia watu kwa kuomba wajiunge na page yako.Page yako itahitaji watu elfu moja (1000) tu hili kuthibitishwa. -Anza kuweka video:Facebook wanalipa kwa video yako tu na wala sio picha,kadri video yako inavyotazamwa ndio huwa unatengeneza pesa ambako watu elfu moja (1k) wakitazama video basi kuanzia hapo video yako itaanza kulipwa. Mambo ya kuzingatia unapowe...