Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 25, 2022

RIPOTI YA KUUNGUA SOKO LA KARUME YAFUNGUA MAZITO

Picha
Dar es salaam Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza kuungua soko la Karume Mwandisi Justin Lukaza ameripoti jumla ya thamani ya fedha zilizotokana na kuungua soko ni zaidi ya bilioni 7.2 huku jumla ya wafanyabiashara 3,090 wakiwa ndio wahaanga wa tukio. Mwenyekiti wa ulinzi wa mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni mkuu wa mkoa Amos Makala ,ametaja chanzo cha moto kuwa ni mshumaa uliowashwa na watumiaji wa dawa za kulevya (mateja).Makala ameelekeza polisi kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa kwasababu wanajulikana.

MARIO BALOTELI AITWA TENA ITALIA

Picha
Roma. Mchezaji wa klabu ya Adana Demirspor  ,Mario Baloteli (31) amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia. Mario Baloteli ambaye kwa mara ya mwisho alijumuishwa mwaka 2018 anarudi rasmi kwenye timu ya taifa ya Azzuri kwenye playoff kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar. Duniani imekuwa habari kubwa kutokana na tabia za "super" ambapo aliwahi kushikana na kocha wake Roberto Mancini akiwa Manchester City ambaye pia ndio kocha wa sasa wa kikosi cha Azurri.

KILICHOMUONDOA MUKOKO TONOMBE YANGA HIKI HAPA

Picha
 Dar es salaam. Klabu ya Yanga hivi leo imetangaza kuachana na mkongomani Mukoko Tonombe.Kupitia mitandao ya kijamii klabu hio ya mitaa ya jangwani ilithibitisha kuachana na kiungo huyo fundi. Mukoko ambaye ameitumikia klabu ya Yanga takribani msimu mmoja na nusu anaripotiwa kujiunga na klabu ya Tp Mazembe ya DRC . Taarifa za uchunguzi wetu zimebaini Mukoko alijikuta kwenye hali ya sintofahamu na mabosi wake tangu alipoonyesha utovu wa nidhamu kwenye Azam Sports Federation  fainali huko Kigoma ni baada ya kumfanyia rafu mbaya mchezaji John Bocco hatua ambayo ilipelekea Mukoko kulimwa kadi nyekundu.Hatua hio ya Mukoko kufanya makosa hayo ilipelekea maisha yake ndani ya klabu ya Yanga kuwa mabaya.