DIAMOND NA ALIKIBA MAMBO SAFI

Dar es salaam.



Msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz akipiga stori kwenye kipindi cha "THE SWITCH" cha radio WASAFI FM inayorusha matangazo yake kutokea Mbezi beach ,Dar es salaam.

Diamond Platinumz amesema hana wasiwasi wa kufanya kolabo na msanii Alikiba na hana ugomvi nae isipokuwa ni maneno ya mashabiki ,wanaowashindanisha kwenye mziki.

Akipiga stori ,alijibu baadhi ya maswali ya watangazaji wa redio hiyo waliotaka kufahamu kama ana bifu na msanii mwenzake Alikiba,Diamond alikataa akidai kwamba kumshindanisha na wasanii wa ndani ni kuikosea tasnia ya mziki wa Bongo Fleva na watanzania pia.Diamond ambaye alifika kutambulisha EP yake ya "FOA" kwa mashabiki wake amejitambulisha kuwa sasa ni msanii namba 3 kwa Afrika.

ila kuna mawazo ambayo watanzania tunatakiwa tuyafute ,ili wewe uonekane mkubwa lazima ugombane na mtu,Mimi sina noma halafu kila mtu namuheshimu kwa upande wake"
Diamond Platinumz kwasasa anatoka na EP ya FOA yenye nyimbo kama Fresh📝📣somebody🎍Sona🎃Melody🎊Loyal🎏Fine 🎂Oka🎆Mtasubiri📟Wonder.

Alikiba na Diamond wamekuwa kwenye bifu Kali toka mwaka 2011 huku ikitajwa kuwa Diamond alikataa kutoa wimbo wa "lala salama" wa kumshirikisha Alikiba na kinyume chake alitoa wimbo wenye sauti yake.Viongozi mbalimbali akiwepo aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania, hayati John Pombe Magufuli alijitahidi kuwapatanisha hasa kwa kuwaalika kwenye dhifa za kitaifa lakini wawili hawa bado haikuwa rahisi kupatana.Uwepo wa ugomvi wao umekuwa wa manufaa kwa kujipatia mashabiki yaani Timu Kiba na Timu Mond.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI