Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 6, 2022

DIAMOND NA ZUCHU WAPATA PIGO

Picha
Dar es salaam. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imezuia wimbo wa Diamond ft Zuchu ujulikanao kama "mtasubiri" kwa muda kutokana na kipande cha video kuonekana na tafsiri mbaya. Katika taarifa ya mamlaka hiyo nchini imeeleza video ya wimbo huo ina kipande kinachoonyesha Zuchu ni mwana kwaya ambaye yuko kanisani anaimba na ghafla anapigiwa simu na kupokea simu wakati anaimba kwenye kwaya. Kutokana na kitendo hicho kipande, hali imekuwa ya sintofahamu kwa waumini wa dini ya Ukiristo ambao wametafsiri kama udhalilishaji. Aidha,mamlaka imemtaka mmiliki wa wimbo huo Diamond kurekebisha maudhui ya video hiyo na pia kuomba watu na vyombo vya habari kutosambaza video hiyo.

MWAFRIKA AULA USEMAJI IKULU YA MAREKANI

Picha
Washington. Ofisi ya Rais wa Marekani imemtangaza bi Karina Jean-Pierre kuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani yaani White House.Mwanamke huyu mweusi anachukua nafasi hiyo kwenye mamlaka ya juu kwenye serikali ya Marekani baada ya kuwa mtu wa karibu wa Rais Biden. Katika taarifa yake Rais Biden amemsifia kwa uzoefu,talanta na uadilifu akisema kwamba anajivunia kutangaza kuteuliwa kwake kama Katibu wa habari wa Ikulu hiyo huku msemaji wa sasa wa Ikulu hiyo Jen Psaki nae akiandika kwenye mtandao wake wa Twitter amemtaja Pierre kama mwanamke wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo ndani ya Ikulu ya Marekani. Jean Pierre  mwenye umri wa miaka 44 amewahi kufanya kazi kwenye kampeni za Barack Obama mnamo mwaka 2008 na 2012 kabla ya kujiunga na timu ya Joe Biden 2020 ndani ya Ikulu ya Marekani.

KURASA ZA MAGAZETI YA MEI 6

Picha