Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 23, 2022

YANGA YAKAA MGUU SAWA UBINGWA LIGI YA TANZANIA

Picha
Dar es salaam. Mzunguko duru la kwanza la ligi ya NBC PREMIER LEAGUE umemalizika leo kwenye uwanja wa Manungu Complex ukishuhudia wababe wa Dar es salaam timu ya wananchi Yanga wakiwachapa Mtibwa Sugar magoli mawili (2) bila majawabu. Mchezo huo uliokuwa wa mwisho kwenye ufungaji wa mzunguko wa kwanza wa ligi uliitimishwa kwa magoli ya Saido Ntabazonkiza (45+) na Fiston Mayele (67)  na kuihakikishia Yanga kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 39 ikifuatiwa na Simba Sports club yenye jumla ya pointi 31. Wakati mzunguko wa kwanza unamalizika imeshuhudiwa mchezaji wa timu ya Namungo     Reliants Lusajo akiongoza kwa kuziona nyavu huku akiwa na magoli 7 akifatiwa na Mwaikenda na     Mayele wote wakiwa na jumla ya magoli 7.Mpaka sasa jumla ya michezo 120 imechezwa huku jumla ya magoli yakiwa ni 228. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kuanzia tarehe 27/02/2022 kwa hatua ya raundi ya pili ya michuano hiyo ya ligi ya NBC.

MKE WA BILIONEA MSUYA AKIRI KUMUUA WIFI YAKE

Picha
Dar as salaam. Mke wa aliekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha ,marehemu Erasto Msuya ,Miriam Mrita ameeleza sababu na namna alivyohusika na mauaji ya wifi yake Aneth Msuya. Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji hayo ya wifi yake huyo  Aneth aliyeuawa mei 25,2016 kwa kuchinjwa shingoni akiwa kwake Kibada Kigamboni ,jijini Dar es salaam amekiri kuhusika na mauaji hayo katika maelezo yake. Katika maelezo hayo, Miriam ameeleza kuwa aliamua kumuua wifi yake kwasababu alikuwa anamfuata fuata katika suala la usimamizi wa mirathi ya mumewe marehemu bilionea Msuya na kwamba katika kutekeleza mauaji basi alimkodi mtu aliemlipa sh 20 milioni. Mbali na Miriam mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018 inayosikilizwa na Jaji Edwin Kakolaki Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam ni mfanyabiashara Revocatus Myella. Maelezo hayo ya Miriam yalisomwa mahakamani hapo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka,WP sajenti Mwajuma ,aliyemhoji mshtakiwa huy

KURASA ZA MAGAZETI LEO FEBRUARY 23/02/2022

Picha

CHELSEA YAICHAPA LILLE 2-0

Picha
London. Timu ya Chelsea ya kaskazini mwa London imefanikiwa kuichapa klabu ya Lille ya nchini Ufaransa jumla ya magoli mawili (2) kwa sifuri (0) kwenye mkondo wa kwanza wa michuano ya klabu bingwa Ulaya yaani UEFA. Lille mabingwa wa ligi ya Ufaransa msimu wa 2021-22 wamekubali kupoteza kwa idadi ya magoli mawili yakifungwa kwa ustadi na Kai Havertz na Christian Pulisic. Kabla ya mchezo uo ,kocha wa Chelsea alinukuliwa na vyombo vya habari akikiri kuwa washambuliaji wa Chelsea wanapata wakati mgumu kufunga. Kwingineko,Vilabu vya Juventus ya Italia na Villarreal ya nchini Uhispania vimetoshana nguvu ni baada ya kutoka kwa sare ya 1-1.