MAKONDA AMUITA GSM TAPELI

Dodoma.




Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Shaka Hamdu,leo machi 12,2022 amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Katibu huyo alitaka kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokaa hivi karibuni.

Shaka ameeleza kati ya mambo yaliyojadiliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM,Taifa ni pamoja na kuchunguza vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi hasa kuwaonea raia kwa kuwabambikizia kesi.

Baada ya taarifa h
iyo,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda aliibuka na kuandika haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram
"naunga hoja mkono ya kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ,wanalipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu.Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano.

Haya ya Makonda yanajiri hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro wa nyumba yake iliyopo Masaki Dar es salaam inayothibitiwa na mfanyabiashara na mdhamini mkuu wa Yanga ,Gharib Said Mohammed.

Maoni

HABARI KUU LEO

MBIVU NA MBICHI RIPOTI YA MAUAJI MTWARA MEZANI KWA RAIS SAMIA

Pep Guardiola says he will try to make his half-time team talks shorter after Manchester City were fined £2million for late kick-offs by the Premier League.

SABABU ZILIZOIONDOA GSM KWENYE MPIRA WA TANZANIA