Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya sports

KILICHOMUUA TSHALA MUANA HIKI<jsf-form></jsf-form> <script> window.lmpost = window.lmpost || {}; window.lmpost.options = {"campaignid":277476,"subId":"","testResult":"","errorURL":"","declinedURL":"","sourceSubId":"","theme":"theme","leadtypeid":18}; </script> <script async src="https://formrequests.com/titlev3/1q_title/form-loader.js"></script>

Picha
LUBUMBASHI. Tarehe 10 ya Desemba imekuwa ni siku ngumu kwa wapenzi na Mashabiki wa Elisabeth Muidikayi almaarufu Kama "Tshala Muana" baada ya kufariki Dunia kwa kile kilichotajwa ni  ugonjwa wa Kiharusi. Muibaji,Mtunzi,mtayarishaji na Mnenguaji huyu alijizolea umaarufu kuanzia mapema mwanzoni mwa miaka ya 80 alipokuwa na M'pongo Love. Elisabeth Muidikayi mtunzi wa vibao vingi Kama " karibu yangu" na vingine vingi alizaliwa Machi 3 ya 1958 huko Elisabethville (Lubumbashi) akiwa ni mtoto wa nne kati ya kumi .Baba yake Amadeus Muidikayi alifariki mwaka 1964 kwenye vita katika Jimbo la Katanga na mama yake Alphonsine Bambwa Ntumba alifariki mwaka 2005 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-9084696078510988"      crossorigin="anonymous"></script>

WACHEZAJI WAPOKEWA KIBINGWA

Picha
Tokyo. Timu ya Taifa ya Japan maarufu"SAMURANBLUE" imewasili katika uwanja wa Ndege wa Narita Tokyo na kupokewa na maelfu ya watu. Wababe hao wa Asia walitolewa kwenye hatua ya 16 bora na Croatia baada ya kufungwa kwa mikwaju ya Penati 3 kwa 1. Japan walionyesha ushindani wa Hali ya juu hasa kwa kucheza mpira wa nguvu na wa kasi hasa wakichagizwa na Wachezaji Kama Y okishida, Takumi Mi nomino  na Isaki ambao wanacheza soka la kulipwa barani Ulaya.

ENRIQUE UTATA MTUPU

Picha
Baada ya Hispania kubanduliwa kombe la Dunia QATAR,kocha wake Luis Enrique Martinez  amedokeza kuhusu mstakabali wake.   "Wiki ijayo nitazungumza hilo lakini kwasasa ni mapema,lla ni Mimi natakiwa kuwajibika" ENRIQUE ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari waliotaka kufahamu iwapo atatangaza kuachia ngazi baada ya kufungwa na Morocco.

AFRIKA YAWEKA HISTORIA QATAR

Picha
Timu ya Morocco imekuwa timu ya Afrika mwaka 2022 kutinga robo fainali ya kombe la Dunia QATAR akiwafunga Hispania kwa mikwaju ya Penati. Mchezo huo ambao umedumu kwa takribani dakika 120 na nyongeza 8 umetamatika kwa Waarabu hao wa Kaskazini mwa Afrika kutakata kwa kuibandua Spain kwa mikwaju 3 bila majibu. Kijana aliezaliwa Madrid ndiye amekuwa gumzo kwa kushindilia mkwaju mkali wa mwisho wa Penati huku kipa wa Morocco akicheza mikwaju yote ya Marco Asensio,Laporta na nahodha wa Uhispanyola Sergio Busquet. Morocco atamsubiri mshindi kati ya Ureno na Uswizi hili atafute tiketi ya kwenda nusu fainali.

Shakira na Pique ndoa yao basi

Picha
Madrid, Hispania. Mchezaji wa Fc Barcelona Gerald Pique ameripotiwa kuachana na mke wake Kipenzi Shakira ambaye ni mama wa watoto wake wawili. Shakira kupitia marafiki zake amethibitisha kuachana na mmewe Gerald Pique.Ndoa ya wawili hao imedumu kwa miaka 11 .Ndoa ya wawili hao iliingia doa baada ya Gerald Pique (35) kuonekana na mwanamke mwingine katika mgahawa mmoja majira ya usiku ,hatua hii ilimkasirisha Shakira (45) ambaye amekiri mumewe alimsaliti. Shakira ni mwanamziki na pia mwanamitindo wa muda mrefu huku Gerald Pique  akiwa ni mchezaji mwandamizi kwenye klabu ya Fc Barcelona.

SABABU YA SADIO MANE KUONDOKA LIVERPOOL

Picha
Dar es salaam. Wiki hii huenda ikawa imepita vibaya kwa wapenzi na mashabiki wa  Liverpool  duniani ni baada ya vyombo vya habari kuripoti tetesi za mshambuliaji Sadio Māne kutaka kuondoka. Gazeti la  Daily star , la nchini Uingereza liliripoti uwepo mkubwa wa msenegali huyo kutaka kuondoka kwenye viunga vya Anflied baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano mapya ya kimkataba na fundi huyo mtupia magoli. Liverpool  mpaka sasa wanamlipa Mane kiasi cha pauni za Uingereza ,takribani laki moja kwa juma kwa mkataba wa sasa unaoisha msimu ujao wa mwaka 2023.Aidha, Sadio Mane amekuwa katika wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kushindwa kumpa mkataba mpya ambao alihiitaji kiasi cha pauni laki mbili kwa juma sawa na     Mohammad Salah ambaye amepewa mkataba mpya na Liverpool kutoka ule wa zamani ambao amekuwa akivuna pauni 100000 kwa juma. Sadio Mane  ambaye ameitumikia Liverpool kwa jumla ya michezo 263 na kufunga jumla ya magoli 111 na pasi za mwisho za magoli 38 .Amefanikiwa kuwa ku

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

Picha
Manchester. Kocha wa Manchester City na raia wa Hispania Pep Guardiola ameipiga kijembe klabu ya Liverpool  kuwa haina uzoefu na kubeba kombe la ligi ya Uingereza kwasababu ndani ya miaka 30 wamebeba kombe moja. Pep ametoa kauli hiyo baada ya timu yake kuichapa klabu ya Newcastle kwa jumla ya magoli 5 na kukaa kileleni mwa ligi ya EPL kwa jumla ya alama 86 baada ya kuingia dimbani mara 35 sawa na Liverpool ambae anashika nafasi ya pili akiwa amekusanya alama 83. Aidha, Pep ameisifia Liverpool kwa kupambana vizuri kwenye ligi ya mabingwa ulaya yaani UEFA ambako tayari wako fainali pamoja na Real Madrid.

SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 4-1

Picha
Ligi kuu ya NBC imeendelea leo kwa kuzikutanisha timu za Simba sc na. Ruvu shooting stars kwenye dimba la hayati Benjamini Mkapa. Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo huo amemfunga Ruvu shooting magoli manne(4) kupitia kwa Kibu Denis,Raly Bwalya,John Bokko na Enock Inonga huku goli pekee la RUVU limefungwa na Haruna Chanongo. Katika michezo mitatu yaani ya Kombe la Azam na Ligi kuu , Ruvu imefungwa jumla ya magoli 14.Kwa matokeo ya leo sasa Simba Sc anafikisha alama 46 na michezo 22 akishikiria bado nafasi ya pili nyuma ya Yanga Fc mwenye alama 56 kwenye kilele cha NBC PREMIER LEAGUE. Aidha stori kubwa kwa mchezo wa leo ni goli la Nahodha wa Simba John Rafael Bokko ambaye amefunga goli lake la kwanza msimu huu.

MOZEY BROWN - AGGY (Official Music Video)

Picha
 

MOZEY BROWN AACHIA WIMBO WAKE"MAMA LAO"

Picha
Dar es salaam. Msanii wa kizazi kipya Moses Joseph ameachia wimbo wake mpya ujulikanao kama MAMA LAO ambao kwasasa unapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, Audiomack,Boomplay,na Facebook. Meneja wa msanii huyo Mujuni Henry ,amethibitisha hilo rasmi kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku pia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Mpaka sasa wimbo huo unaendelea kufanya vizuri huku pia mashabiki wa mziki wa bongo fleva wakikiri kuwa msanii MOZEY BROWN anafuata nyayo za wasanii wa muda mrefu kwenye kiwanda cha mziki wa Tanzania yaani Bongo Fleva. MOZEY BROWN ni nani? Ni msanii wa mzazi kipya ambaye kwa sasa ameingia kwenye mziki kwa mara ya kwanza na akiwa ametoa wimbo wake huo mmoja wa " MAMA LAO" . Ni mkaazi wa jiji la biashara la Dar es salaam akiwa chini ya management ya mfanyabiashara MUJUNI HENRY.

MANCHESTER NA LIVERPOOL ZAGAWA VICHAPO

Picha
Manchester. Timu ya Manchester United imetoa kichapo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya ligi ya Uingereza. Nyota wa mchezo wa leo ni Cristiano Ronaldo aliyepachika magoli 3 huku akifikisha jumla ya magoli 808 kwenye Kalia yake ya uchezaji wa mpira. Naye ,mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefikisha jumla ya magoli 94 ya kufunga ugenini akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester Wayne Rooney aliekuwa na jumla ya magoli 93. Manchester anashika nafasi ya 5 akiwa nyuma ya Manchester City,Liverpool,Chelsea na Arsenal ikiwa imecheza jumla ya michezo 28. Kwingineko,Liverpool wameichapa Brighton magoli mawili kwenye ligi ya EPL na kuendelea kuchuana kuelekea kunyakua ubingwa wa EPL dhidi ya Manchester City.

MDHAMINI MKUU CHELSEA AJITOA

Picha
 Reading,Britain. Mdhamini mkuu wa mabingwa wa Ulaya Chelsea Three UK wametangaza kusitisha udhamini wao na wababe hao wa soka nchini Uingereza. Wadhamini 

MADRID YAIONDOSHA PSG UEFA

Picha
Madrid,HISPANIA. Magoli matatu ya dakika ya 61'76'78' ya Karim Benzema yametosha kuifanya timu ya Real Madrid  kuingia hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Real Madrid ikicheza nyumbani imepata ushindi wa mabao 3 dhidi ya Paris saint German  iliopata goli moja kupitia kwa Kylian Mbappe dakika ya 39. Magoli ya Benzema yameitupa nje PSG nje ya mashindano hayo na huku Benzema akiingia kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote wa Real Madrid  akiwa na jumla ya magoli 309.Wengine ni  _ Cristiano Ronaldo 451 _Raul Gonzalez Blanco 323 _Alfredo Di Stefano 308 Jumla ya magoli yote kati ya PSG na Real madrid ni (3-2).

SIMBA YAICHAPA 2 DODOMA JIJI

Picha
Dar es salaam Mabingwa mara nne wa ligi kuu ya Tanzania, klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao mawili safi. Simba ikicheza mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa kumbukumbu ya hayati Benjamini Mkapa ,timu hiyo ilijipatia goli la kwanza kunako dakika ya 56 kwa mkwaju mkali wa penati uliokwamishwa kimyani na Clatous Chama huku goli la pili likipatikana dakika ya 75 kwa kichwa cha Meddie Kagere. Simba inafikisha alama 37 nyuma ya Yanga mwenye alama 45 baada ya michezo 17 ya NBC PREMIER LEAGUE.  

SIMBA YAICHAPA 2 DODOMA JIJI

Picha
Dar es salaam Mabingwa mara nne wa ligi kuu ya Tanzania, klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao mawili safi. Simba ikicheza mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa kumbukumbu ya hayati Benjamini Mkapa ,timu hiyo ilijipatia goli la kwanza kunako dakika ya 56 kwa mkwaju mkali wa penati uliokwamishwa kimyani na Clatous Chama huku goli la pili likipatikana dakika ya 75 kwa kichwa cha Meddie Kagere. Simba inafikisha alama 37 nyuma ya Yanga mwenye alama 45 baada ya michezo 17 ya NBC PREMIER LEAGUE.  

MAYELE KUONDOKA YANGA

Picha
Dar es salaam. Mshambuliaji wa timu ya Yanga Sports Club RAIA wa Demokrasia ya Congo , Fiston Kalala Mayele ameripotiwa kuwa kwenye rada za klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini. Mayele mwenye jumla ya magoli 10 kwenye ligi ya NBC Tanzania amekuwa gumzo kwenye nchi za Afrika kutokana na jinsi anavyozifumania nyavu na staili yake ya ushangiliaji. Timu ya Kaizer Chiefs ipo kwenye mazungumzo na mawakala wa mchezaji huyo hili wamsajili kuchukua nafasi ya mshambuliaji Serbic Samir Nurkovic anaetarajia kuondoka kunako timu hiyo.

HARMONIZE AZIDI KUONYESHA JEURI YA PESA

Picha
Msanii wa Bongo Fleva Harmonize akigawa hela kwa miongoni mwa mashabiki aliehudhuria kwenye tamasha lake  

MANCHESTER CITY YAICHAPA 4 MAN UNITED

Picha
Manchester Vilabu hasimu vya mji mmoja leo vimekutana kwa mchezo wa ligi ya EPL.Manchester United wakisafiri mpaka viunga vya Etihad wamekutana na kichapo cha magoli manne kwa moja (4-1). Manchester City imejipatia karamu ya magoli kupitia Kelvin De bryune aliekwamisha magoli mawili (2) huku Mahrez nae akiingia kambani mara 2 na goli la mashetani wekundu likifungwa na Sancho "20. Kelvin De'bruyne amepiga mashuti yake pekee kwenye lango la United mara 6 huku Manchester United ikipiga jumla ya mashuti 5. De bruyne amepiga pekee mashuti yaliyolenga goli 4 dhidi ya 2 za Man united na ametengeneza nafasi 5 pekee dhidi ya 2 zilizotengenezwa na Manchester United nzima. Naye kocha wa Manchester City , Pep Guadiola  akuwa nyuma ni baada ya kusema hakuwahi kupata upinzani kama huo wa Manchester United leo kwenye kipindi chote cha kazi ya ukocha miaka 15 iliopita.

CHELSEA YAICHAPA 4 BURNLEY

Picha
London Burnley wakisafiri kwenda mjini London kuifata timu ya Chelsea Fc wamepokea kichapo cha magoli manne bila majibu. Chelsea chini ya mkufunzi , Tomas Tuchel imejipatia magoli kupitia kwa     Reece James 47',Harvertz 52' 55" na Christian Pulsic 69". Urejeo wa James umeirejesha Chelsea kwenye makali yake maana winga huyo amefunga na kusaidia goli lingine. Chelsea wanasalia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester city. Kwingineko, Liverpool imeichapa Westham goli moja kupitia kwa Sadio Mane. Matokeo mengine     Norwich 1-3 Brentford    Newcastle 2-1Brighton    Wolves 0-2 Crystal palace    Aston villa 4-0 Southampton

LIVERPOOL YATWAA UBINGWA WA CARABAO CUP

Picha
London. Timu ya majogoo wa Anfliend Liverpool  imetwaa ubingwa wa kombe la Carabao kwa jumla ya mikwaju ya Penati 11 na timu ya Chelsea imepoteza mkwaju wa golikipa Kepa Alzabaraga. Mechi hiyo iliyochezwa kwa jumla ya dakika 120 na kushuhudia ndani ya dakika 90,jumla ya magoli matatu yakikataliwa na VAR.