KOFFI OLOMIDE AKUBALI UJIO WA WENGE

Kinshasa DRC

Mwanamziki mkongwe barani Afrika Charles Antonio Mumba Olomide amefurahishwa na hatua ya wanamziki waliounda kundi la WENGE MUSICA au WENGE MUSICA BCBG kuamua kuungana upya katika hatua ya kufufua kundi hilo.Kundi la WENGE MUSICA lilianzishwa na Didier Msika mwaka 1981 likipitia tena kwenye mikono ya JB MPIANA mnamo mwaka 1986 kablà ya kuvunjika mwaka 1997 huku sababu ikitajwa viongozi wake wakuu kutoelewana.

Nguli huyu wa miondoko ya Sokous na Rhumba amesema anapenda kundi hili lirudi upya huku akizungumzia kile ambacho huwa kinatajwa kwamba yeye na Papa Wemba ndio walikuwa watu waliosababisha kundi hilo kufa amesema
nafurahi sana WENGE MUSICA kurudi lakini mimi nilisemwa kuliua kundi hili lakini hiyo ilikuwa vita ya ushindani Wa kimziki na kutafuta ufalme pia wa mziki .


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI