Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 27, 2022

BASHUNGWA ATAKA HALMASHAURI ZOTE KUWA NA MASTER PLAN

Picha
Dar es salaam. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Innocent Bashungwa ametaka halmashauri zote nchini kuwa na master plan na sio tu halmashauri zenye miradi ya maendeleo pekee. Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati akipokea taarifa za TSCP,ULGSP na DMDP kutoka kwa kikundi kazi kilichokuwa kinasimamia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini zilizo chini ya TARURA. Waziri Bashungwa amesisitiza ya kwamba ni lazima halmashauri ziweke mipango ya maeneo kabla hili mabadiliko ya technolojia na saikolojia yasije kuleta changamoto katika mipangilio ya maeneo. Haya yanajiri wakati waziri Bashungwa akiwa katika ziara yake katika mkoa wa Dar as salaam.

RAIS SAMIA AFUNGUA SIRI NZITO ZA MAISHA YAKE

Picha
DODOMA Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ametimiza miaka 62.Rais Samia akiwa kwenye mahojiano kupitia idhaa ya kiswahili ya leo ya Tanzania (TBC) Rais Samia amefungua mengi ya moyoni hasa akijikita kuelezea safari ya kimaisha mpaka kuukwaa urais wa Tanzania. Haya ndio mahojiano ya Rais Samia Suluhu Hassan https://youtu.be/95obq76F_pI

ORODHA YA MABILIONEA WA AFRIKA NA MTANZANIA YUMO.

Picha
Dar es salaam. Orodha ya mabilionea 18 wa Afrika iliotolewa na Forbes inaonyesha Aliko Dangote ni kinara kwa ukwasi wa dola 13.9 bilioni. Dangote ambaye ni mwenyeketi wa Dangote Group amekuwa tajiri namba moja Afrika kwa miaka 13 mfululizo na ikitajwa kwamba utajiri wake umeongezeka mara dufu toka mwaka uliopita.Utajiri wa Dangote ambao kwenye soko la hisa la Nigeria NSE umekuwa ukipanda hii ni kutokana na mauzo ya hisa zake za kampuni ya cement ya DANGOTE CEMENT PLC. Kwenye orodha hii ya mabilionea pia yuko Strive Masiyiwa raia wa Zimbabwe anaeishi Uingereza ambaye taarifa za Forbes zinaeleza yeye utajiri wake umeongezeka mara dufu zaidi ukilinganisha na mabilionea wengine 17.Kupitia kampuni yake ya ECONET AFRICA,ameongeza utajiri wake kutoka $ 1.9bilioni mpaka $ 2.7 billion .Mauzo ya hisa za Econet yalipanda na kufikia 750% kwenye  masoko ya hisa nchini Uingereza. Jumla ya utajiri wa mabilionea wa Afrika ni $ 89 bilioni sawa na wastani wa 4 bilioni kwa mabilionea 18 waliotajwa. Nchi

MCHEZAJI WA MANCHESTER AITUPA TIMU YAKE NJE YA AFRICON

Picha
Yaunde Cameroon Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kusaka bingwa wa kandanda katika bara la Afrika. Misri chini ya nahodha wake Mohammed Salah anaesukuma kandanda kunako klabu ya Liverpool ya nchi Uingereza,ameitimisha kwa kufunga penati ya 5 kati ya 4 za Ivory Coast maarufu "tembo". Mchezo wa Ivory Coast na Misri uliisha kwa dakika 90 za kawaida bila kufungana na 30 za nyongeza kabla ya mikwaju ya penalti kuamuriwa kwa mujibu wa sheria za soka. Ivory coast imejikuta ikitupwa nje ya michuano ni baada ya beki kisiki wa Manchester United Eric Bailly kukosa mkwaju wa penati. Mchezo huu uliongozwa au kuchezeshwa na mwamuzi Jean Jacques Ngambo Ndala wa DRC .