Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 15, 2022

YANGA YATINGA ROBO FAINALI KIBABE

Picha
Dar es salaam Klabu ya Yanga Sports Club  imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la TFF baada ya kuilaza Biashara United  ya mkoani Mara kwa jumla ya magoli mawili (2) kwa moja (1). Yanga ikitakata vema kwenye uwanja wa Mkapa imejipatia magoli yake kupitia kwa Yanic Bangala na Fiston Mayele huku goli pekee la timu ya Biashara United likifungwa na Collins Opare . Yanga inaingia hatua hii huku timu za Azam Fc,Geita Fc,Kagera sugar ,Coastal Union na Polisi Tanzania zikiwa zimeshatangulia kwenye hatua hio.

HAKUNA NDOA YA DIAMOND NA ZUCHU HIKI NDIO KILIFANYIKA

Picha
Dar es salaam. Wasanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz na Zuchu wamefanya shughuli kubwa katika ukumbi wa Mlimani City. Katika tukio hilo lililoteka hisia za watu wengi hasa katika jiji la kibiashara la Dar es salaam  ,wengi walifahamu fika msanii kipenzi cha watu Diamond Platnumz anamuoa msanii wa lebo yake ya WCB   Zuchu. Katika hali ya hisia za watu kwamba ni ndoa kati ya wawili ao lakini mambo yalikuwa ya tofauti ni baada ya kilichohisiwa kuwa ndoa kugeuka maonyesho ya nyimbo tu.

JIFUNZE NAMNA YA KUMPATA MME NA MKE HAPA

Picha
Dar es salaam. Suala la mahusiano limekuwa na changamoto sana kutokana na wengi wanaoingia kutokuwa na uelewa wa jambo lenyewe. Mahusiano yana changamoto ambazo upelekea watu kuwa na visasi ambavyo uzaa vifo,talaka na watoto wa mitaani. Mbinu za kupata Mme na Mke hizi hapa 1.Mtangulize MUNGU : Hapa lazima pawe ni kipaumbele kwasababu mwanzilishi wa ndoa ni MUNGU mwenyewe na ndio anaunganisha watu pia. 2.SHIRIKISHA MTU UNAEMWAMINI: Watu wa kwanza wa kukuletea Mme au Mke ni wazazi wako au mlezi.Wazazi au walezi wanapokuchagulia mke au Mme wao wataangalia mambo haya;- A) Mila na desturi.  Mzazi au mlezi ana uelewa wa suala la ndoa kwahio masuala ya tamaduni atayaangalia .Mchagga atataka kijana au binti amuoe au aolewe na Mchagga mwenzake kwasababu atajua mila na desturi ni kiungo sahihi kwenye ndoa. B) Tabia.Historia ya wazazi wa binti au kijana wataifatilia ambayo huwa inaakisi tabia za binti au kijana anaengia kwenye ndoa. 3.CHAGUA MTU AMBAYE NI WA AINA YAKO.Vijana wengi hili wanalijua