Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 4, 2022

MORRISON ALICHOMFANYIA BOSS WAKE BARBARA HIKI HAPA

Picha
Dar es salaam. Klabu ya Simba imemsimamisha winga wake mghana Bernad Morrison kutokana na utovu wa nidhamu. Kupitia taarifa rasmi ya klabu hio iliotolewa na meneja wa mawasiliano Ahmed Ally ,imethibitika mchezaji huyo alimtolea maneno machafu CEO wa klabu io Barbara Gonzalez . Timu ya Simba ilijipatia ushindi wa magoli 6 dhidi ya Dar City kwenye michuano ya kombe la shirikisho.Baada ya mchezo na timu ya Dar City ,Mtendaji wa klabu hio aliingia vyumba vya kubadilisha nguo ambako alimkumbatia mchezaji Clatos Chota Chama huku mchezaji Morrison nae akitaka kumkumbatia Barbara lakini CEO huyo alikataa hali iliopelekea Morrison kumwambia "acha shobo kwa  Chama".Baada ya kauli hio ambayo Morrison aliisema kwa kiswahili ilizua sintofahamu kati ya viongozi na mchezaji huyo. Simba ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili ya ligi ya NBC TANZANIA huku ikikabiliwa na ratiba ngumu ya mechi za kombe la shirikisho barani Afrika zitakazolindima mfululizo ndani ya mwezi huu wa pili.

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO

Picha
Dar es salaam.

MISRI YAICHAPA CAMEROON 3-1

Picha
Yaoundé. Leo nusu fainali ya pili imechezwa kwenye dimba la Limbe ikiikutanisha miamba wa Afrika Cameroon dhidi ya  Misri. Mechi hii iliochezwa kwa takribani dakika 120 imeamliwa kwa mikwaju ya penati baada ya Misri kupata mikwaju mitatu (3) huku Cameroon ikipata mkwaju mmoja (1). Misri mabingwa mara saba( 7) wa kombe hili wanamfuata Senegal ambaye alitinga hatua ya fainali baada ya kuibandua Burkina Faso magoli matatu (3) dhidi ya moja (1). Misri ametinga fainali kwa kumgaragaza mwenyeji Cameroon huku Kocha wake mkuu Carlos Queroz  akilimwa Kadi nyekundu na huku benchi pia la ufundi likikosa huduma ya kocha msaidizi ambaye pia alifungiwa mechi NNE (4) za mashinda