Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 12, 2022

MANCHESTER NA LIVERPOOL ZAGAWA VICHAPO

Picha
Manchester. Timu ya Manchester United imetoa kichapo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya ligi ya Uingereza. Nyota wa mchezo wa leo ni Cristiano Ronaldo aliyepachika magoli 3 huku akifikisha jumla ya magoli 808 kwenye Kalia yake ya uchezaji wa mpira. Naye ,mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefikisha jumla ya magoli 94 ya kufunga ugenini akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester Wayne Rooney aliekuwa na jumla ya magoli 93. Manchester anashika nafasi ya 5 akiwa nyuma ya Manchester City,Liverpool,Chelsea na Arsenal ikiwa imecheza jumla ya michezo 28. Kwingineko,Liverpool wameichapa Brighton magoli mawili kwenye ligi ya EPL na kuendelea kuchuana kuelekea kunyakua ubingwa wa EPL dhidi ya Manchester City.

KAJALA AFUNGA KUMUOMBEA MONALISA

Picha
Dar es salaam. Frida Masanja au Kajala Masanja ;ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye amemshukru MUNGU baada ya watanzania waliokuwa nchini Ukraine kufanikiwa kuondoka kutokana na vita akiwemo mtoto wa mwigizaji mwenzake ,Monalisa aitwaye Sonia. Kajala anasema kuwa,alifunga na kumuombea Sonia ambaye alikuwa masomoni nchini humo hili aweze kupita salama katika hali iliyotea Ukraine na kwasasa anamshukru MUNGU kwaajili ya Sonia kurudi na kuungana na familia yake akiwa salama.Sonia ni miongoni mwa watanzania waliofanikiwa kuondoka Ukraine wakiwa salama kupitia Urusi. Kajala Masanja akizungumza na Gazeti la IJUMAA ,anasema kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno alichokuwa anapitia Monalisa na yeye kama mzazi anajua machungu aliyoyapitia mwenzake.

MORRISON HANA CHAKE SIMBA

Picha
Dar es salaam. Akizungumza na mashabiki na wanachama wa Simba ,Rais wa heshima wa timu hiyo Mohamed Dewji kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ametolea ufafanuzi mambo mengi likiwepo suala la nidhamu ndani ya timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam. Mohammed Dewji  "Viongozi wetu wananidhamu kubwa ,tunataka kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu .Kama mchezaji atakuwa hana nidhamu basi tutaagana naye .Tunataka kujenga timu yenye nidhamu." Wakati haya yakijiri ni hivi karibuni mchezaji Bernard Morrison alionekana kuwa kwenye msuguano na viongozi wakuu wa Simba akiwepo mtendaji mkuu Barbara Gonzalez. Klabu ya Simba ililazimika kumfungia raia huyo wa Ghana kutocheza mechi na kufanya mazoezi na timu yao lakini baadaye mchezaji huyo alilazimika kuandika barua ya kuomba msamaha,klabu ya Simba ilikubali na kumrudisha kambini ingawa Morrison amekuwa na matukio ya kujirudia ya utovu wa nidhamu tangu aikimbie klabu ya Yanga . Kauli ya Mohammed huenda ikawa taya

ALIKIBA NA SHILOLE SASA NI DAMU DAMU

Picha
Dar es salaam. Wasanii Alikiba na Shilole wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kipindi cha miezi minne ya msuguano. Shilole ambaye ni msanii na mfanyabiashara alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya msanii mwenzake Alikiba kudai Shilole kuhudhuria kwenye shughuli yake bila kualikwa.Kauli hiyo ya Alikiba aliyoitoa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam ilimuibua Shilole alietokwa na maneno mazito aliyoyapost kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Shilole na Alikiba wamekubali kurudi kwenye ukaribu wao wa zamani ni baada ya mwana mama Shilole kusema yeye na Alikiba wamemaliza tofauti zao kijeshi. Alikiba mpaka sasa hajatoa neno kuhusu kauli ya Shilole ingawa wawili ao walionekana kwenye tamasha la MwamiNtale mkoani Kigoma wakiimba na kukumbatiana jukwaani mapema mwezi February.

KURASA ZA MAGAZETI LEO MACHI 12,2022

Picha
Dar es salaam. Mambo vipi Tanzania. Magazeti ya leo yanasomeka hivi,tafadhali endelea kutembelea blog hii kila siku kupata vichwa vya magazeti ya siku husika.