HISTORIA YA MUIMBAJI LATA MANGESHKAR
Makala. Mnamo tarehe 06/02/2022 saa 2:15 usiku katika hospital ya SANDWICH ndipo gwiji Lata Mangeshkar aliaga dunia huko Mumbai India huku dalili zote zikionyesha alikuwa na UVIKO 19 ulioshadidishwa na ugonjwa wa mapafu yaani Nimonia.Taarifa ya Dkt Patel Samudanh aliekuwa anamuangalia takribani siku 19 kabla ya kifo chake.Kwa mujibu wa daktari huyo ,viungo vyote vya mwili wake vilisimama na kukataa kufanya kazi ilipofika saa 2:12 usiku uo wa februari 06 mwaka huu. Lata Mangeshkar alikuwa muimbaji wa nyuma ya pazia (playback singer) ambaye kwa takribani miongo saba (7) mtawalia alitawala masikio na nyoyo za wapenzi wa filamu za kihindi maarufu Bollywood duniani kote. Katika utamaduni wa filamu za kihindi,waimbaji huwa hawaimbi kama tuonavyo bali Casett uwekwa na muigizaji ujifanya tu kuimba kumbe sio kweli na uo ndio utamaduni wa wahindi mpaka leo. Sauti yake Lata Mangeshkar waliemuita kifupi Lata G hutumika kama mvuto wa hisia kwa wapenzi wa filamu za kihindi ambao huusisha...