TYSON FURY AMPA TANO KLITSCHKO

Marekani.



Staa wa uzito wa juu duniani,Tyson Fury,amewaunga mkono mabondia wa Ukraine ,Wladimir Klitschko na Vital Klitschko kwa kitendo cha kujitoa kuipambania nchi yao katika vita inayoendelea dhidi ya Urusi.

staa huyo alisema"
"kuna sheria mbili duniani,mpende mwanamke wako na pambania nchi yako ,hivyo wacha wapambanie nchi yao jambo ambalo ni muhimu,mimi niko pamoja nao.

Kwa sababu unaweza kutafuta pesa halafu mwisho wa siku ukashindwa kurudi nyumbani na kutamba,hivyo ni bora kwenda kupambania nchi yako.

Vijana endeleeni kupambana bila kuchoka na wala msikate tamaa,msijisalimishe, tuko pamoja "

Mwaka 2015,Fury alifanikiwa kupambana na bondia Wladimir Klitschko na kushinda.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI