DIAMOND NA ZUCHU WAPATA PIGO

Dar es salaam.




Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imezuia wimbo wa Diamond ft Zuchu ujulikanao kama "mtasubiri" kwa muda kutokana na kipande cha video kuonekana na tafsiri mbaya.

Katika taarifa ya mamlaka hiyo nchini imeeleza video ya wimbo huo ina kipande kinachoonyesha Zuchu ni mwana kwaya ambaye yuko kanisani anaimba na ghafla anapigiwa simu na kupokea simu wakati anaimba kwenye kwaya.



Kutokana na kitendo hicho kipande, hali imekuwa ya sintofahamu kwa waumini wa dini ya Ukiristo ambao wametafsiri kama udhalilishaji.



Aidha,mamlaka imemtaka mmiliki wa wimbo huo Diamond kurekebisha maudhui ya video hiyo na pia kuomba watu na vyombo vya habari kutosambaza video hiyo.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI