MADRID YAIONDOSHA PSG UEFA

Madrid,HISPANIA. Magoli matatu ya dakika ya 61'76'78' ya Karim Benzema yametosha kuifanya timu ya Real Madrid kuingia hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya. Real Madrid ikicheza nyumbani imepata ushindi wa mabao 3 dhidi ya Paris saint German iliopata goli moja kupitia kwa Kylian Mbappe dakika ya 39. Magoli ya Benzema yameitupa nje PSG nje ya mashindano hayo na huku Benzema akiingia kwenye orodha ya wafungaji wa muda wote wa Real Madrid akiwa na jumla ya magoli 309.Wengine ni _ Cristiano Ronaldo 451 _Raul Gonzalez Blanco 323 _Alfredo Di Stefano 308 Jumla ya magoli yote kati ya PSG na Real madrid ni (3-2).