Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 7, 2022

SABABU ZILIZOIONDOA GSM KWENYE MPIRA WA TANZANIA

Picha
Dar es salaam. Taarifa ya kushtua kwenye mpira wa Tanzania imetoka leo ni baada ya kampuni ya GSM kuamua kukaa pembeni kama mdhamini mwenza wa mpira wa miguu Tanzania. T   aarifa ya Afisa mkuu wa biashara wa GSM Allan Chanjo imesema ,wao kama wadhamini wanajitoa kuwa wadhamini wenza wa ligi ya NBC PREMIER LEAGUE. Taarifa za GSM kujiondoa kwenye udhamini zinajiri ikiwa ni miezi miwili na wiki mbili tangu waingie mkataba na TFF novemba 23 2021. Wakata sakata hili likijiri TFF imethibitisha kupokea taarifa ya GSM na kuahidi kutoa ufafanuzi baadae.Kupitia mazungumzo na kituo cha WASAFI RADIO  ,mmoja wa viongozi kwenye bodi ya ligi bw Kizuguto amekiri kupokea taarifa pia kutoka kwa katibu mkuu wa TFF. Udhamini wa GSM ulipata nakama kwa siku za mwanzoni baada ya klabu ya SIMBA FC kutaka maelezo zaidi juu ya mkataba wa udhamini wa TFF na GSM ambako Simba kupitia kwa mtendaji mkuu wake     Barbara walikataa jezi za Simba kuchapwa nembo ya GSM . Taarifa za ndani kutoka chanzo kimoja zimethibiti

KURASA ZA MAGAZETI LEO

Picha
Dar es salaam

SENEGAL WAICHAPA MISRI 4-2 WAKITWAA UBINGWA AFRIKA

Picha
Yaoundé Cameroon. Timu ya taifa ya Senegal imetwaa ubingwa wa michuano ya kombe la mataifa Afrika. Senegal chini ya mkufunzi Aliou Cisse imetwaa ubingwa huo ikiwa ni mara ya kwanza tangu michuano hii kuanzishwa. Senegal yenye nyota  kama Sadio Mane ilijaribu karata ya ubingwa huu miaka mitatu iliopita na kuishia kushika nafasi ya pili ni  baada ya kufungwa kwenye fainali na Algeria. Mchezo wa fainali umechezwa katika uwanja wa Olembe kwenye mji mkuu wa Yaounde.

AJINYONGA NA KUACHA KICHANGA CHA MIEZI MITATU

Picha
GEITA. Katika hali isiyokuwa ya kawaida ,mwanamke mmoja aliejulikana kwa majina ya Naomi Ilyumba (22) mkaazi wa mamlaka ya mji mdogo Katoro Geita katika mkoa wa Geita amekutwa amejinyonga kwenye choo. Afisa mtendaji wa kata ya Katoro bw Selemani Maushi amekiri kutokea kwa tukio hilo.Mwanamke huyu alijinyongea kwenye nyumba ya wageni ijulikanayo kama Mwananzoka inayomilikiwa na Siki Mwananzoka ambaye pia alikuwa ni mme wa bi Naomi. Katika hali ya kuhuzunisha Naomi amejiua huku akiacha mtoto mchanga wa miezi mitatu (3) na huku chanzo cha kujiua kikitajwa ni wivu Wa mapenzi.