Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 10, 2022

HISTORIA YA MAISHA YA PAPA WEMBA

Picha
Mwanamziki Papa Wemba alizaliwa 14 Juni 1949 na kufariki 24 April 2016,alizaliwa Lubefu Zaire ya Zamani. Papa Wemba ni mwamba Wa Mziki Wa Sukus na anafahamika Dunia kwa mtindo wake Wa uvaaji na utanashati ujulikanao kwa lugha ya Kifaransa yaani la Saperé. Umaarufu zaidi Wa Papa Wemba ulitokana na kundi lake la mziki la Viva la Musica  Mwaka 1969,Papa Wemba akiwa na hakina Nyoko Longo,Bimi Ombale,Moloko Leilei na Vuela Somo walikuwa vijana wa mwanzo watanashati na walijiunga na kuanzisha kundi la mziki la Zaiko Langa langa lililokuwa likiimba mziki Wa Sukusi.Tofauti ya mziki wa Sukusi na Rhumba la wakati huo wa makundi ya TP OK Jazz au Afriza International  ni kwamba mziki huu unaenda kasi mno.Mziki huu ulianzishwa na vijana waliochoshwa na mziki wa Rhumba wa kukumbatiana mwanzo mwisho bila jasho ,wao walitaka toka nukta ya kwanza ya kuanza mziki ni kucheza mwanzo mwisho. Sukusi  ni kizazi cha nne cha mziki wa Rhumba kutoka Zaire,utamaduni waliopitia vizazi vinne na kuunda kile kizazi k