JINSI YA KUONGEZA KIPATO

Uchumi. Dunia ya leo ya mapinduzi ya nne ya viwanda ni tofauti na Dunia ya enzi za Ujima ambapo binadamu alitegemea kutembea kutafuta mahitaji yake kama matunda,mizizi na nyama kwa kuokota. Kwenye Dunia ya leo inakuhitaji kuwekeza katika maarifa zaidi ,ambapo utafungua akili na kuona fursa na kuziendea na pia utahitaji kuanza kuwekeza .Uwekezaji una maana pana ingawa watu wengi hufahamu uwekezaji ni pesa pekee ambalo sio kweli.Uwekezaji ni sawa na kumwambia Fundi wa nguo ashone suti,fundi akiambiwa suti yeye hupata picha kamili kwenye akili yake kwahiyo fundi mpaka anatoa hiyo nguo basi tunasema nguo inayoonekana ni picha ya kilichomo ndani ya fundi. Uwekezaji ni mawazo kwanza na ndio pesa hufuatia. Namna ya kuongeza kipato