Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 9, 2022

MAKAMPUNI 47 YAONDOKA URUSI

Picha
Kiev. Wakati leo ikiwa ni siku ya 10 tangu Urusi iishambulie nchi ya Ukraine kijeshi,Urusi imeendelea kupata vikwazo vikali huku pia shinikizo likiwa ni kubwa . Urusi ambaye ni mzalishaji wa pili wa mafuta yote duniani nyuma ya Saudia Arabia na mzalishaji wa gesi ya asili kinara duniani pia mzalishaji wa vipuri anaenda kupata vikwazo ambavyo huenda akapata arhari za haraka .Nchi ya Marekani kupitia kwa Rais wake Joe Bidden  ametangaza marufuku ya mafuta na gesi  ya Urusi huku pia nchi ya Uingereza nayoikipiga marufuku mafuta ya Urusi lakini Ujerumani imekataa kuiwekea Urusi vikwazo. Wakati hayo yakijiri baadhi ya makampuni makubwa yamesitisha huduma zake nchini Urusi ambayo ina takribani raia milioni 144.Mpaka sasa jumla ya makampuni 47 yamefunga huduma zake nchini humo yakiwemo DHL,PUMA,BOEING,VISA,HEINEKEN,YOUTUBE,FEDEX,MICROSOFT,GOOGLE,UNILIVER,COCACOLA,PEPSI,MCDONALD,PIZZA HUB,BP,MAERSK,AIR RNB,UPS,TOYOTA, VW na FORD. Mpaka sasa Urusi chini ya msemaji wake Dimitri alikuwa ametoa

MAYELE KUONDOKA YANGA

Picha
Dar es salaam. Mshambuliaji wa timu ya Yanga Sports Club RAIA wa Demokrasia ya Congo , Fiston Kalala Mayele ameripotiwa kuwa kwenye rada za klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini. Mayele mwenye jumla ya magoli 10 kwenye ligi ya NBC Tanzania amekuwa gumzo kwenye nchi za Afrika kutokana na jinsi anavyozifumania nyavu na staili yake ya ushangiliaji. Timu ya Kaizer Chiefs ipo kwenye mazungumzo na mawakala wa mchezaji huyo hili wamsajili kuchukua nafasi ya mshambuliaji Serbic Samir Nurkovic anaetarajia kuondoka kunako timu hiyo.

CHECHE ZA MBOWE LEO IRINGA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Picha
Iringa. Mwenyekiti wa taifa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa uraiani leo kwa siku ya nne toka atoke gerezani àmekutana na wanawake wa BAWACHA mkoa wa Iringa kwenye siku ya wanawake duniani. Mbowe ambaye ametoa hotuba yake kwa tahadhali kubwa amesema "CHADEMA haikwamishi mipango ya serikali bali serikali inakwama ikiiona CHADEMA". Mbowe ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi .