Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BONGO NEWS

KOFFI OLOMIDE AKUBALI UJIO WA WENGE

Picha
Kinshasa DRC Mwanamziki mkongwe barani Afrika Charles Antonio Mumba Olomide amefurahishwa na hatua ya wanamziki waliounda kundi la  WENGE MUSICA au WENGE MUSICA BCBG kuamua kuungana upya katika hatua ya kufufua kundi hilo.Kundi la WENGE MUSICA lilianzishwa na Didier Msika mwaka 1981 likipitia tena kwenye mikono ya JB MPIANA mnamo mwaka 1986 kablà ya kuvunjika mwaka 1997 huku sababu ikitajwa viongozi wake wakuu kutoelewana. Nguli huyu wa miondoko ya Sokous na Rhumba amesema anapenda kundi hili lirudi upya huku akizungumzia kile ambacho huwa kinatajwa kwamba yeye na Papa Wemba ndio walikuwa watu waliosababisha kundi hilo kufa amesema nafurahi sana WENGE MUSICA kurudi lakini mimi nilisemwa kuliua kundi hili lakini hiyo ilikuwa vita ya ushindani Wa kimziki na kutafuta ufalme pia wa mziki .

HISTORIA YA MAISHA YA PAPA WEMBA

Picha
Mwanamziki Papa Wemba alizaliwa 14 Juni 1949 na kufariki 24 April 2016,alizaliwa Lubefu Zaire ya Zamani. Papa Wemba ni mwamba Wa Mziki Wa Sukus na anafahamika Dunia kwa mtindo wake Wa uvaaji na utanashati ujulikanao kwa lugha ya Kifaransa yaani la Saperé. Umaarufu zaidi Wa Papa Wemba ulitokana na kundi lake la mziki la Viva la Musica  Mwaka 1969,Papa Wemba akiwa na hakina Nyoko Longo,Bimi Ombale,Moloko Leilei na Vuela Somo walikuwa vijana wa mwanzo watanashati na walijiunga na kuanzisha kundi la mziki la Zaiko Langa langa lililokuwa likiimba mziki Wa Sukusi.Tofauti ya mziki wa Sukusi na Rhumba la wakati huo wa makundi ya TP OK Jazz au Afriza International  ni kwamba mziki huu unaenda kasi mno.Mziki huu ulianzishwa na vijana waliochoshwa na mziki wa Rhumba wa kukumbatiana mwanzo mwisho bila jasho ,wao walitaka toka nukta ya kwanza ya kuanza mziki ni kucheza mwanzo mwisho. Sukusi  ni kizazi cha nne cha mziki wa Rhumba kutoka Zaire,utamaduni waliopitia vizazi vinne na kuunda kile kizazi k

MOZEY BROWN - AGGY (Official Music Video)

Picha
 

MOZEY BROWN AACHIA WIMBO WAKE"MAMA LAO"

Picha
Dar es salaam. Msanii wa kizazi kipya Moses Joseph ameachia wimbo wake mpya ujulikanao kama MAMA LAO ambao kwasasa unapatikana kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, Audiomack,Boomplay,na Facebook. Meneja wa msanii huyo Mujuni Henry ,amethibitisha hilo rasmi kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram huku pia kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Mpaka sasa wimbo huo unaendelea kufanya vizuri huku pia mashabiki wa mziki wa bongo fleva wakikiri kuwa msanii MOZEY BROWN anafuata nyayo za wasanii wa muda mrefu kwenye kiwanda cha mziki wa Tanzania yaani Bongo Fleva. MOZEY BROWN ni nani? Ni msanii wa mzazi kipya ambaye kwa sasa ameingia kwenye mziki kwa mara ya kwanza na akiwa ametoa wimbo wake huo mmoja wa " MAMA LAO" . Ni mkaazi wa jiji la biashara la Dar es salaam akiwa chini ya management ya mfanyabiashara MUJUNI HENRY.

DIAMOND NA ZUCHU WAPATA PIGO

Picha
Dar es salaam. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imezuia wimbo wa Diamond ft Zuchu ujulikanao kama "mtasubiri" kwa muda kutokana na kipande cha video kuonekana na tafsiri mbaya. Katika taarifa ya mamlaka hiyo nchini imeeleza video ya wimbo huo ina kipande kinachoonyesha Zuchu ni mwana kwaya ambaye yuko kanisani anaimba na ghafla anapigiwa simu na kupokea simu wakati anaimba kwenye kwaya. Kutokana na kitendo hicho kipande, hali imekuwa ya sintofahamu kwa waumini wa dini ya Ukiristo ambao wametafsiri kama udhalilishaji. Aidha,mamlaka imemtaka mmiliki wa wimbo huo Diamond kurekebisha maudhui ya video hiyo na pia kuomba watu na vyombo vya habari kutosambaza video hiyo.

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI

 Dar es salaam. Mchezo kati ya klabu ya Yanga na Namungo umemalizika hapa uwanja wa kumbukumbu ya Benjamini Mkapa kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli mawili (2) kwa moja (1). Magoli ya Yanga yamefungwa na Fiston Mayele na Feisal Salim.  Kwingineko, Arsenal ya Uingereza imeibuka na ushindi wa magoli matatu bila majibu. 

DIAMOND NA ALIKIBA MAMBO SAFI

Picha
Dar es salaam. Msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz akipiga stori kwenye kipindi cha "THE SWITCH" cha radio WASAFI FM inayorusha matangazo yake kutokea Mbezi beach ,Dar es salaam. Diamond Platinumz amesema hana wasiwasi wa kufanya kolabo na msanii Alikiba na hana ugomvi nae isipokuwa ni maneno ya mashabiki ,wanaowashindanisha kwenye mziki. Akipiga stori ,alijibu baadhi ya maswali ya watangazaji wa redio hiyo waliotaka kufahamu kama ana bifu na msanii mwenzake Alikiba,Diamond alikataa akidai kwamba kumshindanisha na wasanii wa ndani ni kuikosea tasnia ya mziki wa Bongo Fleva na watanzania pia.Diamond ambaye alifika kutambulisha EP yake ya "FOA" kwa mashabiki wake amejitambulisha kuwa sasa ni msanii namba 3 kwa Afrika. ila kuna mawazo ambayo watanzania tunatakiwa tuyafute ,ili wewe uonekane mkubwa lazima ugombane na mtu,Mimi sina noma halafu kila mtu namuheshimu kwa upande wake" Diamond Platinumz kwasasa anatoka na EP ya FOA yenye nyimbo kama Fresh📝📣so

MAKONDA AMUITA GSM TAPELI

Picha
Dodoma. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Shaka Hamdu,leo machi 12,2022 amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Katibu huyo alitaka kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokaa hivi karibuni. Shaka ameeleza kati ya mambo yaliyojadiliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM,Taifa ni pamoja na kuchunguza vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi hasa kuwaonea raia kwa kuwabambikizia kesi. Baada ya taarifa h iyo,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda aliibuka na kuandika haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram "naunga hoja mkono ya kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ,wanalipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu.Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano. Haya ya Makonda yanajiri hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro wa nyumba yake iliyopo Masaki Dar es salaam inayothibitiwa na mfanyabiashara

KAJALA AFUNGA KUMUOMBEA MONALISA

Picha
Dar es salaam. Frida Masanja au Kajala Masanja ;ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye amemshukru MUNGU baada ya watanzania waliokuwa nchini Ukraine kufanikiwa kuondoka kutokana na vita akiwemo mtoto wa mwigizaji mwenzake ,Monalisa aitwaye Sonia. Kajala anasema kuwa,alifunga na kumuombea Sonia ambaye alikuwa masomoni nchini humo hili aweze kupita salama katika hali iliyotea Ukraine na kwasasa anamshukru MUNGU kwaajili ya Sonia kurudi na kuungana na familia yake akiwa salama.Sonia ni miongoni mwa watanzania waliofanikiwa kuondoka Ukraine wakiwa salama kupitia Urusi. Kajala Masanja akizungumza na Gazeti la IJUMAA ,anasema kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno alichokuwa anapitia Monalisa na yeye kama mzazi anajua machungu aliyoyapitia mwenzake.

ALIKIBA NA SHILOLE SASA NI DAMU DAMU

Picha
Dar es salaam. Wasanii Alikiba na Shilole wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kipindi cha miezi minne ya msuguano. Shilole ambaye ni msanii na mfanyabiashara alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya msanii mwenzake Alikiba kudai Shilole kuhudhuria kwenye shughuli yake bila kualikwa.Kauli hiyo ya Alikiba aliyoitoa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam ilimuibua Shilole alietokwa na maneno mazito aliyoyapost kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Shilole na Alikiba wamekubali kurudi kwenye ukaribu wao wa zamani ni baada ya mwana mama Shilole kusema yeye na Alikiba wamemaliza tofauti zao kijeshi. Alikiba mpaka sasa hajatoa neno kuhusu kauli ya Shilole ingawa wawili ao walionekana kwenye tamasha la MwamiNtale mkoani Kigoma wakiimba na kukumbatiana jukwaani mapema mwezi February.

ALIKIBA NA SHILOLE SASA NI DAMU DAMU

Picha
Dar es salaam. Wasanii Alikiba na Shilole wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kipindi cha miezi minne ya msuguano. Shilole ambaye ni msanii na mfanyabiashara alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya msanii mwenzake Alikiba kudai Shilole kuhudhuria kwenye shughuli yake bila kualikwa.Kauli hiyo ya Alikiba aliyoitoa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam ilimuibua Shilole alietokwa na maneno mazito aliyoyapost kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Shilole na Alikiba wamekubali kurudi kwenye ukaribu wao wa zamani ni baada ya mwana mama Shilole kusema yeye na Alikiba wamemaliza tofauti zao kijeshi. Alikiba mpaka sasa hajatoa neno kuhusu kauli ya Shilole ingawa wawili ao walionekana kwenye tamasha la MwamiNtale mkoani Kigoma wakiimba na kukumbatiana jukwaani mapema mwezi February.