HISTORIA YA MAISHA YA PAPA WEMBA

Mwanamziki Papa Wemba alizaliwa 14 Juni 1949 na kufariki 24 April 2016,alizaliwa Lubefu Zaire ya Zamani.



Papa Wemba ni mwamba Wa Mziki Wa Sukus na anafahamika Dunia kwa mtindo wake Wa uvaaji na utanashati ujulikanao kwa lugha ya Kifaransa yaani la Saperé.
Umaarufu zaidi Wa Papa Wemba ulitokana na kundi lake la mziki la Viva la Musica 

Mwaka 1969,Papa Wemba akiwa na hakina Nyoko Longo,Bimi Ombale,Moloko Leilei na Vuela Somo walikuwa vijana wa mwanzo watanashati na walijiunga na kuanzisha kundi la mziki la Zaiko Langa langa lililokuwa likiimba mziki Wa Sukusi.Tofauti ya mziki wa Sukusi na Rhumba la wakati huo wa makundi ya TP OK Jazz au Afriza International ni kwamba mziki huu unaenda kasi mno.Mziki huu ulianzishwa na vijana waliochoshwa na mziki wa Rhumba wa kukumbatiana mwanzo mwisho bila jasho ,wao walitaka toka nukta ya kwanza ya kuanza mziki ni kucheza mwanzo mwisho.
Sukusi ni kizazi cha nne cha mziki wa Rhumba kutoka Zaire,utamaduni waliopitia vizazi vinne na kuunda kile kizazi kipya cha Sukusi ukijuacho leo.


  

Vita ya pili ya Dunia ndio ilizalisha Rhumba kutoka kwenye mziki wa kilatino ,kilatino ndio mama mzazi wa Rhumba la Congo.Wenyewe mziki huu waliuita Kikumba yaani "kitovu" kutokana na utamaduni ule wa asili wa hakina mama kuvaa vibwaya na ambayo ni nguo ya kufunika kifua na kuacha kitovu wazi.Neno Kumba ni kitovu lakini neno hili linawapa wazungu shida na wakasema Rhumba na ndio ilivyobaki mpaka leo. Mziki huu wa Rhumba na Sukusi ulianza wakati vikundi vikubwa vya mziki wa asili kama Franco na Tp OK Jazz na Tabu Ley vilileta ushindani mkubwa kwenye mziki. Hata hivyo mziki huo wa hakina Franco na Tabu Ley ambao ni wa kizazi cha Tatu ulizaa mziki wa kizazi cha nne ukianzia Zaiko Langalanga ,Detrio Majesi ,Bela Bela,Imperial Bakuba, na vikundi vya Kavasha Lipua Lipua,Kamalee,Tshama Tshama na vikundi vingine vingi vilileta mabadiliko makubwa katika mandhari ya mziki wa Congo .Hata hivyo baada ya mafanikio ya kundi hilo la Zaiko ,Papa Wemba akiwa amepata hilo jina akaanzisha Viva La Musica na wanamziki kama Sungani Verodi,Pepe Bipuli ,Fety Aziza na wapiga gitaa kama Ligo Star na Bongo Wende .

Papa Wemba alianza kurekodi kwenye chapa ya Peter Gabriel ambaye alikuwa mwimbaji wa kundi la The Genesis katika mradi mkubwa wa Afrika ujulikanao kama  Grace Land. Mtindo wa Papa Wemba ulibadilika na kuja kwenye maadhi ya kimagharibi na kutoka na kibao "Yolele". Mwaka 1995 alianzisha makundi mawili ,moja liikwa Matonge ambalo lilikuwa kwao Zaire na lingine barani Ulaya huko Paris akiliita Morokai .Morokai ni neno lenye maana ya Kizazi kipya.Mashabiki wake walimlaumu kwa kuacha maadhi ya mziki wa Congo ndipo aliamua kuachana na mkataba huo wa Record label ya Peter Gabriel na kuamua kurudi kwenye maadhi ya nyumbani ambapo aliingia studio na kutoa album ya " Wake up" na Koffi Olomide mnamo mwaka 1997 ambapo aliwakumbusha wanamziki wa Afrika kurudi na kutukuza vitu vyao badala ya vya magharibi maana ni utumwa.



Akiwa na umaarufu mwingi miongoni mwa wanamziki chipukizi ,wengi alikuwa akiwakaribisha nchi za ughaibuni yeye akidhamini ziara zao ,mwaka 2003 alishukiwa kuhusika kwenye mtandao ambao unadaiwa kuvusha mamia ya waamiaji haramu kutoka DRC hadi Ulaya ,papa Wemba alikamatwa kwake mjini Paris. Hatimaye alipatikana na hatia kwa kosa hilo na alifungwa jela kwa miezi mitatu na nusu na baadae kuachiliwa kwa dhamana .Baada ya hapo alikiri hadharani kuwa tukio hilo lilimpa athari za kisaikolojia .


MAFANIKIO
Papa Wemba ameshinda tuzo nyingi za kimataifa ikiwemo ya Cora ya mwaka 1996 pia ameacha filamu inayoitwa lavì bien"Maisha ni mazuri" ,filamu iliyoshinda tuzo ya Gorgeous de LÅ«  nchini Ubelgiji

KIFO
Mwaka 2016 ,April 24 usiku wa jumamosi alikwenda wilayani Anumabu mjini Abdijan nchini Ivory coast kuhudhuria tamasha la kila mwaka la mziki wa mjini maarufu kama FEMUA yaani Festival of urban music of Anumabu .Akiwa jukwaani Papa Wemba alionekana akiimba kwa bashasha na kurap kama kawaida yake. Kwenye picha za video zilimuonyesha Papa Wemba akipokea Maiki kutoka kwa kijana aliyeingia kwenye jukwaa ,baadae papa Wemba anaweka Maiki mdomoni anaimba maneno kidogo anashindwa kuendelea anaanguka  ghafla.Wakati wa tukio hilo mziki haukusimama uliendelea,yule kijana aliembadilishia maiki anaonekana tena anarudi jukwaani haraka haraka na kuiondoa hiyo maiki na kuelekea kusikojulikana .Baadae mwili wake ulibebwa kwenye Ambulance kwenda hospital ya Highers mjini Abijan na mwili wake ulifika hospitalini hapo saa 6 na 30 usiku ambayo ilikuwa tayari Jumapili,mwili wake ulipofikishwa tayari alikuwa ameshaaga Dunia.Baadae mwili wake ukahifadhiwa Mochwari ya Highers hospital. Misa ya marehemu ilifanyika tarehe 27 mjini Abijan na mkewe mama Marie Zolo wa mazoo aliemuoa mwaka 1970 na kuzaa nae watoto 6 alihudhuria misa hiyo kutoka Kinshasa na baadae kurudi na mwili wa marehemu mumewe kwa ndege siku ya tarehe 1 mwezi Mei.
Rais Kabila alimtunuku heshima kuu ya kitaifa kama kiongozi shujaa wa Jamhuri ya watu wa Congo.Papa Wemba alizikwa Mei 4 mwaka 2016 nyumbani kwao Lubefu mkoa wa Sankulu akiwa na umri wa miaka 66.Kifo cha Papa Wemba kina fanana na kifo cha mama Africa


   Miriam Makeba ambaye nae alifariki tarehe 8 November 2008 akiwa jukwaani akiimba akiwa mjini Castro de tuno nchi Italy. Wote wawili wamefariki wakiwa jukwaani wakifanya kile walichochagua kuwa ndio maisha yao .

Tarehe 24 April mwaka huu Serikali ya Congo imezindua jumba la makumbusho kwaajili ya Papa Wemba ikiwa ni miaka 6 tangu kiongozi huyo wa Jadi wa kijiji cha Morokai afariki Dunia .Hii ndio historia ya panda shuka ya nguli Jules Wembadio Kikumba Pene alimaarufu PAPA WEMBA.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI