Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 25, 2022

ATHARI ZA VITA YA URUSI NA UKRAINE KWENYE MICHEZO

Picha
Dar es salaam. Vita ya Urusi na Ukraine ilioanza tarehe 23/02/2022 imezua sintofahamu kubwa duniani ambapo nchi nyingi zimeonyesha kutofurahishwa na hatua ya majeshi ya Urusi kuivamia na kuipiga Ukraine. Vita hii ambayo dunia inashuhudia haijaacha athari kwingine hata kwenye michezo athari zipo nyingi kama ifuatavyo:- Fainali za Uefa zabadilishwa: Fainali ya Uefa iliyotarajiwa kuchezwa 28 Mei kwenye uwanja wa St Petersburg imeamishiwa nchini Ufaransa kwenye uwanja wa     The stade de France uliopo mjini Paris. Manchester United imetangaza kuvunja mkataba wa udhamini na shirika la ndege la Urusi yaani     AEROFLOT ni baada ya majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine. Timu za Serie A kukaa kimya dakika 5: Ligi ya mpira wa miguu ya Italia yaani Serie A itashuhudia kuanzia leo timu za Milan na Udinese zikikaa kimya kwa dakika 5 kama ishara ya kutaka amani ya UKRAINE. BUNDESILIGA yaweka mabango uwanjani: Usiku wa leo utashuhudia vilabu vya Stuttgart na Hoffenheim vikiingia uwanjani na mabango ya

RAIS VOLODYMYR ZELENSKIY WA UKRAINE ATAJA ATHARI ZA VITA NA URUSI

Picha
Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa taarifa ya athari za shambulio la Urusi kwa nchi yake huku akitaja jumla ya watu 137 kuwa wamepoteza maisha wakiwemo na wanajeshi 10 na mpaka sasa jumla ya majeruhi ni 316. Rais Volodymyr amenukuliwa " leo nimewauliza viongozi 27 wa nchi za Ulaya kuhusu kuhofia shambulizi la Ukraine lakini hakuna aliyejibu ,sisi hatuogopi ,hatuogopi chochote ,hatuogopi kuilinda nchi yetu,hatuwaogopi Urusi na hatuogopi kuongea na Urusi. Familia yangu ,watoto wangu wote ni raia wa Ukraine sio wakimbizi kulingana na taarifa tayari tuna maadui ambapo mimi ndio "target" yao ya kwanza na familia yangu ni "target" namba mbili .Wanataka kuimaliza ikulu"

RAYVANNY NA LOKOLE WAINGIA VITA YA MANENO

Picha
Dar es salaam. Mtangazaji wa kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM ya jiji Dar es salaam  Juma Lokole amejikuta kaenye ugomvi na msanii wa Bongo Fleva Rayvanny. Mtangazaji huyo wakati akitangaza alitoa ushauri kwa msanii Rayvanny kwamba alifanya makosa kwa kuachana na mzazi mwenzake Fahma na kuamua kuwa na mahusiano na mrembo Paula. Kutokana na ushauri huo Rayvanny naye alimjibu mtangazaji huyo kupitia Insta story akimueleza kwamba aachane nae kwasababu yeye na mzazi mwenzake bado wanaheshimiana. ___Zaidi Tazama video

BUSTA RYMES AMPA TANO DIAMOND PLATINUMZ

Picha
Dar es salaam. Msanii na mfanyabiashara kutoka code +255 namaanisha Tanzania,  Diamond Platinumz ameachia video na audio ya wimbo wake GIDI ambapo kupitia mtandao wa Instagram aliandika gidi is out of global . Kupitia ujumbe wake aliouweka kwenye Instagram ,miongoni ya walioweka maoni ni nguli rapa     Basta Rhymes alieweka emoji za moto zipatazo saba (7) kuonyesha kukubali kile anachofanya Diamond Platinumz . Wimbo wa Gidi huenda nao ukawa kwenye viwango vya wimbo wa jeje ambao umekuwa gumzo kwenye klabu nyingi za starehe nchini Marekani.

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO 24/02/2022

Picha

MAREKANI ALIVYOWAINGIZA URUSI NA UKRAINE VITANI

Picha
Minsk. Dunia leo imeshuhudia majeshi ya Urusi yakiishambulia nchi ya Ukraine pande za kaskazini,kusini na mashariki. Mgogoro wa nchi hizi umekuwepo sasa miongo kadhaa kutokana na mwingiliano wa maene kama Donbas,Donetsk  na Lugansk. Maeneo haya ambayo nchi ya Ukraine imekuwa ikiyapigania yawe yake ingawa wakazi wa maeneo haya wanaongea kirusi (Russian) tangu mwaka 2014.Katika mkataba wa mwaka 2015 uliofanyika Belarus wa kutaka maeneo haya yatambulike kama sehemu ya Ukraine  yalishuhudia uasi mkubwa ambao umeligawa taifa hilo tangu enzi za Mapinduzi ya Orange ( Orange Revolution)  aliekuwa Rais wa Ukraine wakati huo Yulia Timoshenko  alieungwa mkono na Urusi na Waziri Mkuu wake Viktor Yanukovych kwenye uchaguzi wa mwaka 2004 ambako rais Yulia Timoshenko alikataa matokeo yaliyompa Yanukovych ushindi ambao nchi za ulaya magharibi zilipongeza mno na hata Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Michael Powell. Kiini cha mgogoro Urusi amekuwa mwiba mkali kwa nchi za magharibi kwa kutambua n