Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 16, 2022

MANCHESTER CITY YASHINDA 5 -0 KWENYE UEFA

Picha
Lisbon ,Ureno. Ligi ya mabingwa Ulaya imeendelea leo katika hatua ya 16 bora katika viwanja vya Paris Saint Germain  na Lisbon . Manchester City wakisafiri ugenini wameichapa Sporting CP magoli matano (5) kwa bila (0).Magoli ya Manchester City ilioko chini ya mkufunzi Pep Guardiola ilijizolea karamu ya magoli kupitia Riyard Mahrez,Bernado Silva (2) ,Phil Foden na Raheem Sterling. Huko nchini Ufaransa mchezo wa Real Madrid na Paris Saint Germain umekamilika kwa PSG kuibuka na ushindi wa goli moja (1) kwa bila (0) ,goli likifungwa na Kyllien Mbappe . Mbappe kwa michezo 53 amechangia magoli 19 na kufunga magoli 32 kwenye michuano hii ya UEFA.