CHELSEA YAICHAPA 4 BURNLEY

London Burnley wakisafiri kwenda mjini London kuifata timu ya Chelsea Fc wamepokea kichapo cha magoli manne bila majibu. Chelsea chini ya mkufunzi , Tomas Tuchel imejipatia magoli kupitia kwa Reece James 47',Harvertz 52' 55" na Christian Pulsic 69". Urejeo wa James umeirejesha Chelsea kwenye makali yake maana winga huyo amefunga na kusaidia goli lingine. Chelsea wanasalia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester city. Kwingineko, Liverpool imeichapa Westham goli moja kupitia kwa Sadio Mane. Matokeo mengine Norwich 1-3 Brentford Newcastle 2-1Brighton Wolves 0-2 Crystal palace Aston villa 4-0 Southampton