Baada ya Hispania kubanduliwa kombe la Dunia QATAR,kocha wake Luis Enrique Martinez amedokeza kuhusu mstakabali wake. "Wiki ijayo nitazungumza hilo lakini kwasasa ni mapema,lla ni Mimi natakiwa kuwajibika" ENRIQUE ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari waliotaka kufahamu iwapo atatangaza kuachia ngazi baada ya kufungwa na Morocco.
Tokyo. Timu ya Taifa ya Japan maarufu"SAMURANBLUE" imewasili katika uwanja wa Ndege wa Narita Tokyo na kupokewa na maelfu ya watu. Wababe hao wa Asia walitolewa kwenye hatua ya 16 bora na Croatia baada ya kufungwa kwa mikwaju ya Penati 3 kwa 1. Japan walionyesha ushindani wa Hali ya juu hasa kwa kucheza mpira wa nguvu na wa kasi hasa wakichagizwa na Wachezaji Kama Y okishida, Takumi Mi nomino na Isaki ambao wanacheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Dar es salaam. Wiki hii huenda ikawa imepita vibaya kwa wapenzi na mashabiki wa Liverpool duniani ni baada ya vyombo vya habari kuripoti tetesi za mshambuliaji Sadio Māne kutaka kuondoka. Gazeti la Daily star , la nchini Uingereza liliripoti uwepo mkubwa wa msenegali huyo kutaka kuondoka kwenye viunga vya Anflied baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano mapya ya kimkataba na fundi huyo mtupia magoli. Liverpool mpaka sasa wanamlipa Mane kiasi cha pauni za Uingereza ,takribani laki moja kwa juma kwa mkataba wa sasa unaoisha msimu ujao wa mwaka 2023.Aidha, Sadio Mane amekuwa katika wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kushindwa kumpa mkataba mpya ambao alihiitaji kiasi cha pauni laki mbili kwa juma sawa na Mohammad Salah ambaye amepewa mkataba mpya na Liverpool kutoka ule wa zamani ambao amekuwa akivuna pauni 100000 kwa juma. Sadio Mane ambaye ameitumikia Liverpool kwa jumla ya michezo 263 na kufunga jumla ya magoli 111 na pasi za m...
Maoni