Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya siasa

KILICHOMUUA TSHALA MUANA HIKI<jsf-form></jsf-form> <script> window.lmpost = window.lmpost || {}; window.lmpost.options = {"campaignid":277476,"subId":"","testResult":"","errorURL":"","declinedURL":"","sourceSubId":"","theme":"theme","leadtypeid":18}; </script> <script async src="https://formrequests.com/titlev3/1q_title/form-loader.js"></script>

Picha
LUBUMBASHI. Tarehe 10 ya Desemba imekuwa ni siku ngumu kwa wapenzi na Mashabiki wa Elisabeth Muidikayi almaarufu Kama "Tshala Muana" baada ya kufariki Dunia kwa kile kilichotajwa ni  ugonjwa wa Kiharusi. Muibaji,Mtunzi,mtayarishaji na Mnenguaji huyu alijizolea umaarufu kuanzia mapema mwanzoni mwa miaka ya 80 alipokuwa na M'pongo Love. Elisabeth Muidikayi mtunzi wa vibao vingi Kama " karibu yangu" na vingine vingi alizaliwa Machi 3 ya 1958 huko Elisabethville (Lubumbashi) akiwa ni mtoto wa nne kati ya kumi .Baba yake Amadeus Muidikayi alifariki mwaka 1964 kwenye vita katika Jimbo la Katanga na mama yake Alphonsine Bambwa Ntumba alifariki mwaka 2005 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.<script async src="https://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js?client=ca-pub-9084696078510988"      crossorigin="anonymous"></script>

AFRIKA YAWEKA HISTORIA QATAR

Picha
Timu ya Morocco imekuwa timu ya Afrika mwaka 2022 kutinga robo fainali ya kombe la Dunia QATAR akiwafunga Hispania kwa mikwaju ya Penati. Mchezo huo ambao umedumu kwa takribani dakika 120 na nyongeza 8 umetamatika kwa Waarabu hao wa Kaskazini mwa Afrika kutakata kwa kuibandua Spain kwa mikwaju 3 bila majibu. Kijana aliezaliwa Madrid ndiye amekuwa gumzo kwa kushindilia mkwaju mkali wa mwisho wa Penati huku kipa wa Morocco akicheza mikwaju yote ya Marco Asensio,Laporta na nahodha wa Uhispanyola Sergio Busquet. Morocco atamsubiri mshindi kati ya Ureno na Uswizi hili atafute tiketi ya kwenda nusu fainali.

MWAFRIKA AULA USEMAJI IKULU YA MAREKANI

Picha
Washington. Ofisi ya Rais wa Marekani imemtangaza bi Karina Jean-Pierre kuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani yaani White House.Mwanamke huyu mweusi anachukua nafasi hiyo kwenye mamlaka ya juu kwenye serikali ya Marekani baada ya kuwa mtu wa karibu wa Rais Biden. Katika taarifa yake Rais Biden amemsifia kwa uzoefu,talanta na uadilifu akisema kwamba anajivunia kutangaza kuteuliwa kwake kama Katibu wa habari wa Ikulu hiyo huku msemaji wa sasa wa Ikulu hiyo Jen Psaki nae akiandika kwenye mtandao wake wa Twitter amemtaja Pierre kama mwanamke wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo ndani ya Ikulu ya Marekani. Jean Pierre  mwenye umri wa miaka 44 amewahi kufanya kazi kwenye kampeni za Barack Obama mnamo mwaka 2008 na 2012 kabla ya kujiunga na timu ya Joe Biden 2020 ndani ya Ikulu ya Marekani.

MAKONDA AMUITA GSM TAPELI

Picha
Dodoma. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Shaka Hamdu,leo machi 12,2022 amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Katibu huyo alitaka kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokaa hivi karibuni. Shaka ameeleza kati ya mambo yaliyojadiliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM,Taifa ni pamoja na kuchunguza vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi hasa kuwaonea raia kwa kuwabambikizia kesi. Baada ya taarifa h iyo,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda aliibuka na kuandika haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram "naunga hoja mkono ya kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ,wanalipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu.Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano. Haya ya Makonda yanajiri hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro wa nyumba yake iliyopo Masaki Dar es salaam inayothibitiwa na mfanyabiashara

MAKAMPUNI 47 YAONDOKA URUSI

Picha
Kiev. Wakati leo ikiwa ni siku ya 10 tangu Urusi iishambulie nchi ya Ukraine kijeshi,Urusi imeendelea kupata vikwazo vikali huku pia shinikizo likiwa ni kubwa . Urusi ambaye ni mzalishaji wa pili wa mafuta yote duniani nyuma ya Saudia Arabia na mzalishaji wa gesi ya asili kinara duniani pia mzalishaji wa vipuri anaenda kupata vikwazo ambavyo huenda akapata arhari za haraka .Nchi ya Marekani kupitia kwa Rais wake Joe Bidden  ametangaza marufuku ya mafuta na gesi  ya Urusi huku pia nchi ya Uingereza nayoikipiga marufuku mafuta ya Urusi lakini Ujerumani imekataa kuiwekea Urusi vikwazo. Wakati hayo yakijiri baadhi ya makampuni makubwa yamesitisha huduma zake nchini Urusi ambayo ina takribani raia milioni 144.Mpaka sasa jumla ya makampuni 47 yamefunga huduma zake nchini humo yakiwemo DHL,PUMA,BOEING,VISA,HEINEKEN,YOUTUBE,FEDEX,MICROSOFT,GOOGLE,UNILIVER,COCACOLA,PEPSI,MCDONALD,PIZZA HUB,BP,MAERSK,AIR RNB,UPS,TOYOTA, VW na FORD. Mpaka sasa Urusi chini ya msemaji wake Dimitri alikuwa ametoa

MTOTO WA RAIS MUSEVENI AJIUZURU JESHINI

Picha
Kampala. Kamanda wa jeshi la Ardhini nchini Uganda (UPDF) Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni ,ametangaza kustaafu kulitumikia jeshi hilo. Luteni Kainerugaba kupitia ukurasa wake wa Twitter  ameandika haya" baada ya kuhudumu kwa miaka 28 katika jeshi letu ,jeshi bora zaidi duniani ,nafurahia kutangaza kwamba nastaafu .Mimi na wanajeshi tumefanikiwa pakubwa ,ninawapenda na kuwaheshimu maofisa wote wamefanikiwa kila siku"     ameandika. Kwa mujibu wa sheria ya Uganda ya kustaafu kujihusisha na shughuli za jeshi ya mwaka 2014 itatakiwa Luteni Jenerali aandike barua ya kuomba kujiuzulu ,ndipo ofisa msemaji atatangaza suala hilo na viongozi wakuu wa jeshi la UPDF watakaa na kujadili barua hiyo.Maombi yakikubalika basi jeshi litaandaa sherehe maalum ya kuwaaga rasmi. Kwa mujibu wa vyombo vya ndani nchini Uganda, huenda Muhoozi Kainerugaba anaelekea kwenye siasa na hivi karibuni alimtembelea Rais Kagame wa Rwanda tukio lililosababisha mpa

SABABU ZA RAIS SAMIA KUKUTANA NA FREEMAN MBOWE

Picha
Rais wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan amekutana na mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe. Rais , Samia ameeleza sababu za kukutana na Mbowe.

MBOWE AKUTANA NA RAIS SAMIA

Picha
Dar es salaam. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe yakiwa ni masaa machache baada ya kiongozi huyo kuachiwa na mahakama ya Divisheni ya makosa ya Jinai na uhujumu uchumi Ikulu jijini Dar es salaam. Mbowe ameachiwa mapema leo ni baada ya mwendesha mashtaka DPP kuamua kuachana na kesi hiyo namba 16/2021 ambayo ilimuweka Mbowe na wenzake watatu ndani  kwa siku 226.

MBOWE NA WENZAKE KUJITETEA LEO

Picha
Dar es salaam. Mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe na wenzake watatu leo wanatarajiwa kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka ya ugaidi yanayowakabili. Hatua hii ni baada ya upande wa jamhuri kufunga ushahidi baada ya kuita mashahidi 13 na mahakama kuu (Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi) kuwakuta na kesi ya kujibu. Utetezi wa Mbowe na wenzake Halfan Hassan,Adam kusekwa na Mohamed Ling'wenye wanaoshtakiwa kupanga kulipua vituo vya mafuta na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama masoko kwa lengo la kuifanya nchi isitawalike ,unasubiriwa kwa shauku kubwa na watu wengi.

PAUL MAKONDA AZIDI KUPETA

Picha
Dar es salaam. Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ,Goodchance Reginald amesema mteja wake hakuwa amepewa wito wa kufika mahakamani zaidi ya kuziona habari hizo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Wakili Reginald ameyasema hayo leo katika mahakama ya Kinondoni jijini Dar es salaam na kuomba mahakama impe muda zaidi mteja wake ili kuwakilisha hati kinzani dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na mwandishi wa habari ,    Saed Kubenea ya kutaka kibali cha kumfutia kesi ya jinai. Kufuatia maombi hayo ,Hakimu mkazi Aron Lyamuya anayesikiliza shauri hilo ,amesema mahakama hiyo inampa Makonda siku 21 kuwasilisha hati hizo kinzani dhidi ya maombi ya kumfutia kesi ya jinai yaliyowasilishwa na Kubenea.

MAREKANI ALIVYOWAINGIZA URUSI NA UKRAINE VITANI

Picha
Minsk. Dunia leo imeshuhudia majeshi ya Urusi yakiishambulia nchi ya Ukraine pande za kaskazini,kusini na mashariki. Mgogoro wa nchi hizi umekuwepo sasa miongo kadhaa kutokana na mwingiliano wa maene kama Donbas,Donetsk  na Lugansk. Maeneo haya ambayo nchi ya Ukraine imekuwa ikiyapigania yawe yake ingawa wakazi wa maeneo haya wanaongea kirusi (Russian) tangu mwaka 2014.Katika mkataba wa mwaka 2015 uliofanyika Belarus wa kutaka maeneo haya yatambulike kama sehemu ya Ukraine  yalishuhudia uasi mkubwa ambao umeligawa taifa hilo tangu enzi za Mapinduzi ya Orange ( Orange Revolution)  aliekuwa Rais wa Ukraine wakati huo Yulia Timoshenko  alieungwa mkono na Urusi na Waziri Mkuu wake Viktor Yanukovych kwenye uchaguzi wa mwaka 2004 ambako rais Yulia Timoshenko alikataa matokeo yaliyompa Yanukovych ushindi ambao nchi za ulaya magharibi zilipongeza mno na hata Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Michael Powell. Kiini cha mgogoro Urusi amekuwa mwiba mkali kwa nchi za magharibi kwa kutambua n

JINSI YA KUJIPATIA HELA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

Picha
BIASHARA. Mtandao wa kijamii wa Facebook ni mmoja ya mitandao mikubwa ya kijamii duniani ukiwa na takribani watumiaji bilioni 4. Mtandao huu unaomilikiwa na kampuni ya META iliopo chini ya bilionea kijana Mark Zuckerberg. Mtandao huu ni miongoni mwa mitandao ya kampuni hii ya META ambayo pia inamiliki Whatsapp ,   Instagram na Messenger. NAMNA YA KUTENGENEZA PESA FACEBOOK Facebook kama ulivyo mtandao wa kibiashara huwa unatoa fursa ya watumiaji wake kunufaika na mtandao huu. Hili utengeneze pesa kwanza fungua 1)  Facebook page: Eneo hili upatikana kwenye kushoto mwa ukurasa wa facebook. -Baada ya kufungua page ,vutia watu kwa kuomba wajiunge na page yako.Page yako itahitaji watu elfu moja (1000) tu hili kuthibitishwa. -Anza kuweka video:Facebook wanalipa kwa video yako tu na wala sio picha,kadri video yako inavyotazamwa ndio huwa unatengeneza pesa ambako watu elfu moja (1k) wakitazama video basi kuanzia hapo video yako itaanza kulipwa.     Mambo ya kuzingatia unapoweka video kwenye Fac

Rais MWINYI APONGEZA TEKNOLOJIA YA KUPIMA CORONA "EDE COVID SCANNER"

Picha
Zanzibar. Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya kwanza Afrika kutumia teknolojia ya mashine ya kupima UVIKO (EDE COVID SCANNERS) kutokana na azma yake ya kuimarisha sekta ya utalii ambayo ndio tegemeo kubwa la uchumi wa Zanzibar  Rais Dkt Mwinyi aliyasema hayo leo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa kimataifa na kitaifa kufuatia matukio makubwa yaliyotokea leo hapa nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume likiwemo kuanza tena kwa safari za ndege ya "Fly Dubai" kutoka umoja wa nchi za kiarabu (UAE) ,pamoja na uzinduzi wa matumizi ya mashine ya (EDE COVID SCANNERS) ya kupima UVIKO 19. Alisema kuwa hatua hiyo itapunguza matatizo ambayo wasafiri wanayapata na kusisitiza kwamba ni muhimu serikali kufanya kila juhudi katika kurudisha watalii hapa Zanzibar ambapo ndege ya "Fly Dubai" itakuwa inakuja mara mbili kwa siku.

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO

Picha
Dar es salaam  

VITUKO VYA PASTOR KURIA MKUSH

Picha

KIMPA KISANGAMENI -Lyrics

Picha
Kimpa Kisangameni. Huu ni wimbo wenye tafsiri ya " Kuwa makini na maajabu" .Ni wimbo ambao Franco Luambo Makiadi alikuwa akimtaadhalisha mama yake. Msaada zaidi wa tafsiri fungua hapa  https://www.facebook.com/100063508488919/posts/350155837111363/?app=fbl

WAZIRI NAPE ATOA UFAFANUZI SUALA LA VIFURUSHI ATOA UAMUZI HUU MZITO

Picha
Dar es salaam. Waziri wa mawasiliano ,habari na teknolojia Moses Nape Nauye ametolea ufafanuzi suala la gharama za vifurushi. Akifanya mahojiano na shirika la utangazaji Tanzania  (TBC) ,Waziri Nape ameeleza nia ya dhati ilio nayo serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu ya kuweka unafuu wa gharama za simu .

WAZIRI NAPE ATOLEA UFAFANUZI SUALA LA VIFURUSHI

Picha

BASHUNGWA ATAKA HALMASHAURI ZOTE KUWA NA MASTER PLAN

Picha
Dar es salaam. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Innocent Bashungwa ametaka halmashauri zote nchini kuwa na master plan na sio tu halmashauri zenye miradi ya maendeleo pekee. Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati akipokea taarifa za TSCP,ULGSP na DMDP kutoka kwa kikundi kazi kilichokuwa kinasimamia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini zilizo chini ya TARURA. Waziri Bashungwa amesisitiza ya kwamba ni lazima halmashauri ziweke mipango ya maeneo kabla hili mabadiliko ya technolojia na saikolojia yasije kuleta changamoto katika mipangilio ya maeneo. Haya yanajiri wakati waziri Bashungwa akiwa katika ziara yake katika mkoa wa Dar as salaam.

RAIS SAMIA AFUNGUA SIRI NZITO ZA MAISHA YAKE

Picha
DODOMA Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ametimiza miaka 62.Rais Samia akiwa kwenye mahojiano kupitia idhaa ya kiswahili ya leo ya Tanzania (TBC) Rais Samia amefungua mengi ya moyoni hasa akijikita kuelezea safari ya kimaisha mpaka kuukwaa urais wa Tanzania. Haya ndio mahojiano ya Rais Samia Suluhu Hassan https://youtu.be/95obq76F_pI