MBOWE NA WENZAKE KUJITETEA LEO

Dar es salaam.



Mwenyekiti wa CHADEMA ,Freeman Mbowe na wenzake watatu leo wanatarajiwa kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka ya ugaidi yanayowakabili.

Hatua hii ni baada ya upande wa jamhuri kufunga ushahidi baada ya kuita mashahidi 13 na mahakama kuu (Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi) kuwakuta na kesi ya kujibu.

Utetezi wa Mbowe na wenzake Halfan Hassan,Adam kusekwa na Mohamed Ling'wenye wanaoshtakiwa kupanga kulipua vituo vya mafuta na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama masoko kwa lengo la kuifanya nchi isitawalike ,unasubiriwa kwa shauku kubwa na watu wengi.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI