MWAFRIKA AULA USEMAJI IKULU YA MAREKANI

Washington.


Ofisi ya Rais wa Marekani imemtangaza bi Karina Jean-Pierre kuwa msemaji wa Ikulu ya Marekani yaani White House.Mwanamke huyu mweusi anachukua nafasi hiyo kwenye mamlaka ya juu kwenye serikali ya Marekani baada ya kuwa mtu wa karibu wa Rais Biden.



Katika taarifa yake Rais Biden amemsifia kwa uzoefu,talanta na uadilifu akisema kwamba anajivunia kutangaza kuteuliwa kwake kama Katibu wa habari wa Ikulu hiyo huku msemaji wa sasa wa Ikulu hiyo Jen Psaki nae akiandika kwenye mtandao wake wa Twitter amemtaja Pierre kama mwanamke wa kwanza mweusi kushika wadhifa huo ndani ya Ikulu ya Marekani.


Jean Pierre mwenye umri wa miaka 44 amewahi kufanya kazi kwenye kampeni za Barack Obama mnamo mwaka 2008 na 2012 kabla ya kujiunga na timu ya Joe Biden 2020 ndani ya Ikulu ya Marekani.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI