MTOTO WA RAIS MUSEVENI AJIUZURU JESHINI

Kampala.



Kamanda wa jeshi la Ardhini nchini Uganda (UPDF) Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni ,ametangaza kustaafu kulitumikia jeshi hilo.

Luteni Kainerugaba kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika haya"baada ya kuhudumu kwa miaka 28 katika jeshi letu ,jeshi bora zaidi duniani ,nafurahia kutangaza kwamba nastaafu .Mimi na wanajeshi tumefanikiwa pakubwa ,ninawapenda na kuwaheshimu maofisa wote wamefanikiwa kila siku" 


  ameandika.

Kwa mujibu wa sheria ya Uganda ya kustaafu kujihusisha na shughuli za jeshi ya mwaka 2014 itatakiwa Luteni Jenerali aandike barua ya kuomba kujiuzulu ,ndipo ofisa msemaji atatangaza suala hilo na viongozi wakuu wa jeshi la UPDF watakaa na kujadili barua hiyo.Maombi yakikubalika basi jeshi litaandaa sherehe maalum ya kuwaaga rasmi.

Kwa mujibu wa vyombo vya ndani nchini Uganda, huenda Muhoozi Kainerugaba anaelekea kwenye siasa na hivi karibuni alimtembelea Rais Kagame wa Rwanda tukio lililosababisha mpaka wa Uganda na Rwanda wa Gatuna kufunguliwa tangu ulipofungwa miaka minne iliyopita na pia ndani ya chama cha baba yake cha NLM ana ushawishi mkubwa.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI