Rais MWINYI APONGEZA TEKNOLOJIA YA KUPIMA CORONA "EDE COVID SCANNER"

Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Zanzibar imekuwa ni nchi ya kwanza Afrika kutumia teknolojia ya mashine ya kupima UVIKO (EDE COVID SCANNERS) kutokana na azma yake ya kuimarisha sekta ya utalii ambayo ndio tegemeo kubwa la uchumi wa Zanzibar 



Rais Dkt Mwinyi aliyasema hayo leo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa kimataifa na kitaifa kufuatia matukio makubwa yaliyotokea leo hapa nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume likiwemo kuanza tena kwa safari za ndege ya "Fly Dubai" kutoka umoja wa nchi za kiarabu (UAE) ,pamoja na uzinduzi wa matumizi ya mashine ya (EDE COVID SCANNERS) ya kupima UVIKO 19.



Alisema kuwa hatua hiyo itapunguza matatizo ambayo wasafiri wanayapata na kusisitiza kwamba ni muhimu serikali kufanya kila juhudi katika kurudisha watalii hapa Zanzibar ambapo ndege ya "Fly Dubai" itakuwa inakuja mara mbili kwa siku.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI