MAKAMPUNI 47 YAONDOKA URUSI

Kiev.



Wakati leo ikiwa ni siku ya 10 tangu Urusi iishambulie nchi ya Ukraine kijeshi,Urusi imeendelea kupata vikwazo vikali huku pia shinikizo likiwa ni kubwa .

Urusi ambaye ni mzalishaji wa pili wa mafuta yote duniani nyuma ya Saudia Arabia na mzalishaji wa gesi ya asili kinara duniani pia mzalishaji wa vipuri anaenda kupata vikwazo ambavyo huenda akapata arhari za haraka .Nchi ya Marekani kupitia kwa Rais wake Joe Bidden  ametangaza marufuku ya mafuta na gesi  ya Urusi huku pia nchi ya Uingereza nayoikipiga marufuku mafuta ya Urusi lakini Ujerumani imekataa kuiwekea Urusi vikwazo.

Wakati hayo yakijiri baadhi ya makampuni makubwa yamesitisha huduma zake nchini Urusi ambayo ina takribani raia milioni 144.Mpaka sasa jumla ya makampuni 47 yamefunga huduma zake nchini humo yakiwemo DHL,PUMA,BOEING,VISA,HEINEKEN,YOUTUBE,FEDEX,MICROSOFT,GOOGLE,UNILIVER,COCACOLA,PEPSI,MCDONALD,PIZZA HUB,BP,MAERSK,AIR RNB,UPS,TOYOTA, VW na FORD.

Mpaka sasa Urusi chini ya msemaji wake Dimitri alikuwa ametoa masharti 3 kwa nchi ya Ukraine ikiwemo ya Ukraine kuweka kipengele kwenye katiba ya nchi yao kutojiunga na NATO ,pili UKRAINE ikubali kuyatambua majimbo matatu na jimbo la Crimea kama maeneo halali ya Urusi.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI