JINSI YA KUJIPATIA HELA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK

BIASHARA.

Mtandao wa kijamii wa Facebook ni mmoja ya mitandao mikubwa ya kijamii duniani ukiwa na takribani watumiaji bilioni 4.



Mtandao huu unaomilikiwa na kampuni ya META iliopo chini ya bilionea kijana Mark Zuckerberg.Mtandao huu ni miongoni mwa mitandao ya kampuni hii ya META ambayo pia inamiliki Whatsapp , Instagram na Messenger.

NAMNA YA KUTENGENEZA PESA FACEBOOK

Facebook kama ulivyo mtandao wa kibiashara huwa unatoa fursa ya watumiaji wake kunufaika na mtandao huu.

Hili utengeneze pesa kwanza fungua 1) Facebook page:Eneo hili upatikana kwenye kushoto mwa ukurasa wa facebook.
-Baada ya kufungua page ,vutia watu kwa kuomba wajiunge na page yako.Page yako itahitaji watu elfu moja (1000) tu hili kuthibitishwa.
-Anza kuweka video:Facebook wanalipa kwa video yako tu na wala sio picha,kadri video yako inavyotazamwa ndio huwa unatengeneza pesa ambako watu elfu moja (1k) wakitazama video basi kuanzia hapo video yako itaanza kulipwa.
   Mambo ya kuzingatia unapoweka video kwenye Facebook Page.
_Weka video ambayo umeizalisha mwenyewe:Mtandao wa Facebook kama ilivyo mitandao mingi huwa wanaangalia suala la haki miliki (copyrights).Suala hili linaweza kusababisha page yako kufungiwa.Kwenye video haki miliki ziko kwenye Audio (ala za mziki) na Video (mwonekano wa video).
_Jinsi ya kupata pesa zako kutoka Facebook:Hapa Facebook wakiona umetimiza matakwa yao watakutumia Fomu uijaze na baada ya kuijaza watakuthibitisha kwa kukutumia pesa zako kwa njia za kadi kama Master card.

2) Sambaza Video zako:Hapa inategemea ni video za mtandao gani kama ni youtube ,Spotify,Netflix,Boomplay.Video hizi zikiingia kwenye kurasa za facebook mfano makundi huwa zinawafikia watazamaji wengi kwasababu mtandao huu ni mtandao ambao una watumiaji wengi.

3) Uza biashara yako.Wengi wa wajasiriamali na wafanyabiashara wanatumia mtandao huu kuuza bidhaa zao .Ni rahisi kuona matangazo ya makampuni makubwa kama Coca Cola ,Pepsi ,Airtel na Vodacom kwenye simu yako kupitia mtandao wa facebook.Wengi hutumia mbinu ya Ads ambayo hutoa uharaka wa kupata wateja na huduma hii ulipiwa.

Makala hii kwa mwendelezo unaweza kuwasiliana na mwandishi kwa email ya magejoel20@gmail.com

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI