Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2022

HIZI NDIZO SABABU ZA WASANII WA WASAFI KUTOLIPWA NA COSOTA

Picha
Dar as salaam. Serikali kupitia mamlaka ya haki miliki COSOTA imetaja sifa za msanii ambaye ana sifa ya kupata mirahaba kupitia kwao. Sababu zilizotajwa na mamlaka hio ni pamoja na msanii kutakiwa kujisajili COSOTA   ndio atapata sifa za kupata mapato yake.Kupitia mamlaka hio imetajwa kwamba pia matumizi ya kazi ya msanii ndio itaamua msanii atapata mgao wa kiasi gani? Kwasababu zilizotolewa na COSOTA  basi zimetoa mwelekeo wa kampuni ya WCB kukosa mgao wa fedha za mirahaba kwa wasanii wao kutokana na wasanii wa lebo hio kuwa na migogoro na vituo vingi vya habari kutokucheza kazi zao. 

MAGAZETI YA LEO

Picha
Dar es salaam.

Harmonize FT Otile Brown - WOMAN (video Lyrics)

Picha

Harmonize FT Otile Brown - WOMAN (video Lyrics)

Picha

YANGA 1 vs MBAO 0 | GOLI PEKEE LA MAYELLE

Picha

KIMPA KISANGAMENI -Lyrics

Picha
Kimpa Kisangameni. Huu ni wimbo wenye tafsiri ya " Kuwa makini na maajabu" .Ni wimbo ambao Franco Luambo Makiadi alikuwa akimtaadhalisha mama yake. Msaada zaidi wa tafsiri fungua hapa  https://www.facebook.com/100063508488919/posts/350155837111363/?app=fbl

ALIKIBA-UTU (official video lyrics)

Picha
Dar es salaam. Msanii wa mziki wa bongo fleva Alikiba ameachia hit song inayokwenda kwa jina la "utu". Video ya wimbo iko tayari pia ambako Alikiba amethibitisha hilo kwenye mtandao wake wa Instagram. Alikiba ameandika kwamba shooting za video zimefanyika kwenye Mlima Kilimanjaro na eneo la ziwa Duluti lililopo mkoani Arusha

COSOTA HAIJATOA MGAO KWA WCB

Picha
Dar es salaam. Katika hali isiyotarajiwa mamlaka ya kusimamia haki za umiliki wa kazi za sanaa nchini COSOTA imeshindwa kutoa mgao wa fedha kwa kundi la WCB ambalo liko chini ya msanii Diamond Platinum. Mgao huo wa fedha umetoka serikalini kama mrabaha. Majina ya waliopata mgao ni :- 1.Mt Cecilia (Arusha)-Tsh 8.739 ml 2.Alikiba-Tsh mil 7.588 3.Rose Muhando_Tsh 5.79 4.Ambwene Yesaya-tsh 5.64 5.Emanuel Mgogo- Tsh 5.6 6.Christina Shusho- Tsh 4.5 7.Martha Mwaipaja- Tsh 4.2 8.Ambwene Mwasongwe- Tsh 3.43 9.Nandy-Tsh 2.61 10.Maua Sama -Tsh 1.83 11.Sarafina-Tsh 1.83

KURASA ZA MAGAZETI LEO JANUARY 29

Picha
Dar es salaam. Vichwa vya magazeti

ZARRI ATISHIA KUWASHTAKI WANAOMCHAFUA MITANDAONI

Picha
Johannesburg. Zarri the bosslady ameonya wale wote ambao wanatumia jina lake mitandaoni kuwashtaki.Hii inajiri baada ya mwanamziki na mwanamitindo wa Marekani Cardi B kumshinda mzalishaji wa maudhui kwenye mtandao wa youtube kwenye kesi iliolindima kwenye mahakama moja nchini Marekani.Kwenye hukumu ya kesi hio imeamriwa mshtakiwa kumlipa Cardi B zaidi ya bilioni 7 za Tanzania. Kufuatia mkasa huo wa Marekani nae Zarri ametumia mwanya huo kuwaonya wote wanaotumia jina lake vibaya kwenye mitandao ya kijamii.

WAZIRI NAPE ATOA UFAFANUZI SUALA LA VIFURUSHI ATOA UAMUZI HUU MZITO

Picha
Dar es salaam. Waziri wa mawasiliano ,habari na teknolojia Moses Nape Nauye ametolea ufafanuzi suala la gharama za vifurushi. Akifanya mahojiano na shirika la utangazaji Tanzania  (TBC) ,Waziri Nape ameeleza nia ya dhati ilio nayo serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu ya kuweka unafuu wa gharama za simu .

WAZIRI NAPE ATOLEA UFAFANUZI SUALA LA VIFURUSHI

Picha

BASHUNGWA ATAKA HALMASHAURI ZOTE KUWA NA MASTER PLAN

Picha
Dar es salaam. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa Innocent Bashungwa ametaka halmashauri zote nchini kuwa na master plan na sio tu halmashauri zenye miradi ya maendeleo pekee. Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati akipokea taarifa za TSCP,ULGSP na DMDP kutoka kwa kikundi kazi kilichokuwa kinasimamia fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa barabara za mijini na vijijini zilizo chini ya TARURA. Waziri Bashungwa amesisitiza ya kwamba ni lazima halmashauri ziweke mipango ya maeneo kabla hili mabadiliko ya technolojia na saikolojia yasije kuleta changamoto katika mipangilio ya maeneo. Haya yanajiri wakati waziri Bashungwa akiwa katika ziara yake katika mkoa wa Dar as salaam.

RAIS SAMIA AFUNGUA SIRI NZITO ZA MAISHA YAKE

Picha
DODOMA Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ametimiza miaka 62.Rais Samia akiwa kwenye mahojiano kupitia idhaa ya kiswahili ya leo ya Tanzania (TBC) Rais Samia amefungua mengi ya moyoni hasa akijikita kuelezea safari ya kimaisha mpaka kuukwaa urais wa Tanzania. Haya ndio mahojiano ya Rais Samia Suluhu Hassan https://youtu.be/95obq76F_pI

ORODHA YA MABILIONEA WA AFRIKA NA MTANZANIA YUMO.

Picha
Dar es salaam. Orodha ya mabilionea 18 wa Afrika iliotolewa na Forbes inaonyesha Aliko Dangote ni kinara kwa ukwasi wa dola 13.9 bilioni. Dangote ambaye ni mwenyeketi wa Dangote Group amekuwa tajiri namba moja Afrika kwa miaka 13 mfululizo na ikitajwa kwamba utajiri wake umeongezeka mara dufu toka mwaka uliopita.Utajiri wa Dangote ambao kwenye soko la hisa la Nigeria NSE umekuwa ukipanda hii ni kutokana na mauzo ya hisa zake za kampuni ya cement ya DANGOTE CEMENT PLC. Kwenye orodha hii ya mabilionea pia yuko Strive Masiyiwa raia wa Zimbabwe anaeishi Uingereza ambaye taarifa za Forbes zinaeleza yeye utajiri wake umeongezeka mara dufu zaidi ukilinganisha na mabilionea wengine 17.Kupitia kampuni yake ya ECONET AFRICA,ameongeza utajiri wake kutoka $ 1.9bilioni mpaka $ 2.7 billion .Mauzo ya hisa za Econet yalipanda na kufikia 750% kwenye  masoko ya hisa nchini Uingereza. Jumla ya utajiri wa mabilionea wa Afrika ni $ 89 bilioni sawa na wastani wa 4 bilioni kwa mabilionea 18 waliotajwa. Nchi

MCHEZAJI WA MANCHESTER AITUPA TIMU YAKE NJE YA AFRICON

Picha
Yaunde Cameroon Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kusaka bingwa wa kandanda katika bara la Afrika. Misri chini ya nahodha wake Mohammed Salah anaesukuma kandanda kunako klabu ya Liverpool ya nchi Uingereza,ameitimisha kwa kufunga penati ya 5 kati ya 4 za Ivory Coast maarufu "tembo". Mchezo wa Ivory Coast na Misri uliisha kwa dakika 90 za kawaida bila kufungana na 30 za nyongeza kabla ya mikwaju ya penalti kuamuriwa kwa mujibu wa sheria za soka. Ivory coast imejikuta ikitupwa nje ya michuano ni baada ya beki kisiki wa Manchester United Eric Bailly kukosa mkwaju wa penati. Mchezo huu uliongozwa au kuchezeshwa na mwamuzi Jean Jacques Ngambo Ndala wa DRC .

RIPOTI YA KUUNGUA SOKO LA KARUME YAFUNGUA MAZITO

Picha
Dar es salaam Mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza kuungua soko la Karume Mwandisi Justin Lukaza ameripoti jumla ya thamani ya fedha zilizotokana na kuungua soko ni zaidi ya bilioni 7.2 huku jumla ya wafanyabiashara 3,090 wakiwa ndio wahaanga wa tukio. Mwenyekiti wa ulinzi wa mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni mkuu wa mkoa Amos Makala ,ametaja chanzo cha moto kuwa ni mshumaa uliowashwa na watumiaji wa dawa za kulevya (mateja).Makala ameelekeza polisi kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa kwasababu wanajulikana.

MARIO BALOTELI AITWA TENA ITALIA

Picha
Roma. Mchezaji wa klabu ya Adana Demirspor  ,Mario Baloteli (31) amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Italia. Mario Baloteli ambaye kwa mara ya mwisho alijumuishwa mwaka 2018 anarudi rasmi kwenye timu ya taifa ya Azzuri kwenye playoff kuelekea michuano ya kombe la dunia nchini Qatar. Duniani imekuwa habari kubwa kutokana na tabia za "super" ambapo aliwahi kushikana na kocha wake Roberto Mancini akiwa Manchester City ambaye pia ndio kocha wa sasa wa kikosi cha Azurri.

KILICHOMUONDOA MUKOKO TONOMBE YANGA HIKI HAPA

Picha
 Dar es salaam. Klabu ya Yanga hivi leo imetangaza kuachana na mkongomani Mukoko Tonombe.Kupitia mitandao ya kijamii klabu hio ya mitaa ya jangwani ilithibitisha kuachana na kiungo huyo fundi. Mukoko ambaye ameitumikia klabu ya Yanga takribani msimu mmoja na nusu anaripotiwa kujiunga na klabu ya Tp Mazembe ya DRC . Taarifa za uchunguzi wetu zimebaini Mukoko alijikuta kwenye hali ya sintofahamu na mabosi wake tangu alipoonyesha utovu wa nidhamu kwenye Azam Sports Federation  fainali huko Kigoma ni baada ya kumfanyia rafu mbaya mchezaji John Bocco hatua ambayo ilipelekea Mukoko kulimwa kadi nyekundu.Hatua hio ya Mukoko kufanya makosa hayo ilipelekea maisha yake ndani ya klabu ya Yanga kuwa mabaya.