ORODHA YA MABILIONEA WA AFRIKA NA MTANZANIA YUMO.

Dar es salaam.




Orodha ya mabilionea 18 wa Afrika iliotolewa na Forbes inaonyesha Aliko Dangote ni kinara kwa ukwasi wa dola 13.9 bilioni. Dangote ambaye ni mwenyeketi wa Dangote Group amekuwa tajiri namba moja Afrika kwa miaka 13 mfululizo na ikitajwa kwamba utajiri wake umeongezeka mara dufu toka mwaka uliopita.Utajiri wa Dangote ambao kwenye soko la hisa la Nigeria NSE umekuwa ukipanda hii ni kutokana na mauzo ya hisa zake za kampuni ya cement ya DANGOTE CEMENT PLC.



Kwenye orodha hii ya mabilionea pia yuko Strive Masiyiwa raia wa Zimbabwe anaeishi Uingereza ambaye taarifa za Forbes zinaeleza yeye utajiri wake umeongezeka mara dufu zaidi ukilinganisha na mabilionea wengine 17.Kupitia kampuni yake ya ECONET AFRICA,ameongeza utajiri wake kutoka $ 1.9bilioni mpaka $ 2.7 billion .Mauzo ya hisa za Econet yalipanda na kufikia 750% kwenye


 masoko ya hisa nchini Uingereza.

Jumla ya utajiri wa mabilionea wa Afrika ni $ 89 bilioni sawa na wastani wa 4 bilioni kwa mabilionea 18 waliotajwa.

Nchi zilizoingiza mabilionea ni Nigeria (3),Misri (5),Afrika kusini (5),Tunisia (2),Morocco (1),Tanzania (1) na Zimbabwe (1).

Jarida linalotangaza mabilionea la Forbes hupima utajiri kwa kuangalia hisa na pia mitambo au viwanda anavyomiliki mhusika.


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI