MCHEZAJI WA MANCHESTER AITUPA TIMU YAKE NJE YA AFRICON

Yaunde Cameroon

Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya kusaka bingwa wa kandanda katika bara la Afrika.


Misri chini ya nahodha wake Mohammed Salah anaesukuma kandanda kunako klabu ya Liverpool ya nchi Uingereza,ameitimisha kwa kufunga penati ya 5 kati ya 4 za Ivory Coast maarufu "tembo".

Mchezo wa Ivory Coast na Misri uliisha kwa dakika 90 za kawaida bila kufungana na 30 za nyongeza kabla ya mikwaju ya penalti kuamuriwa kwa mujibu wa sheria za soka.
Ivory coast imejikuta ikitupwa nje ya michuano ni baada ya beki kisiki wa Manchester United Eric Bailly kukosa mkwaju wa penati.


Mchezo huu uliongozwa au kuchezeshwa na mwamuzi Jean Jacques Ngambo Ndala wa DRC .




Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI