KILICHOMUONDOA MUKOKO TONOMBE YANGA HIKI HAPA


 Dar es salaam.

Klabu ya Yanga hivi leo imetangaza kuachana na mkongomani Mukoko Tonombe.Kupitia mitandao ya kijamii klabu hio ya mitaa ya jangwani ilithibitisha kuachana na kiungo huyo fundi.

Mukoko ambaye ameitumikia klabu ya Yanga takribani msimu mmoja na nusu anaripotiwa kujiunga na klabu ya Tp Mazembe ya DRC .

Taarifa za uchunguzi wetu zimebaini Mukoko alijikuta kwenye hali ya sintofahamu na mabosi wake tangu alipoonyesha utovu wa nidhamu kwenye Azam Sports Federation  fainali huko Kigoma ni baada ya kumfanyia rafu mbaya mchezaji John Bocco hatua ambayo ilipelekea Mukoko kulimwa kadi nyekundu.Hatua hio ya Mukoko kufanya makosa hayo ilipelekea maisha yake ndani ya klabu ya Yanga kuwa mabaya.



Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI