Shakira na Pique ndoa yao basi

Madrid, Hispania.



Mchezaji wa Fc Barcelona Gerald Pique ameripotiwa kuachana na mke wake Kipenzi Shakira ambaye ni mama wa watoto wake wawili.

Shakira kupitia marafiki zake amethibitisha kuachana na mmewe Gerald Pique.Ndoa ya wawili hao imedumu kwa miaka 11 .Ndoa ya wawili hao iliingia doa baada ya Gerald Pique (35) kuonekana na mwanamke mwingine katika mgahawa mmoja majira ya usiku ,hatua hii ilimkasirisha Shakira (45) ambaye amekiri mumewe alimsaliti.



Shakira ni mwanamziki na pia mwanamitindo wa muda mrefu huku Gerald Pique akiwa ni mchezaji mwandamizi kwenye klabu ya Fc Barcelona.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI