SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 4-1


Ligi kuu ya NBC imeendelea leo kwa kuzikutanisha timu za Simba sc na. Ruvu shooting stars kwenye dimba la hayati Benjamini Mkapa.

Simba akiwa ni mwenyeji wa mchezo huo amemfunga Ruvu shooting magoli manne(4) kupitia kwa Kibu Denis,Raly Bwalya,John Bokko na Enock Inonga huku goli pekee la RUVU limefungwa na Haruna Chanongo.

Katika michezo mitatu yaani ya Kombe la Azam na Ligi kuu ,Ruvu imefungwa jumla ya magoli 14.Kwa matokeo ya leo sasa Simba Sc anafikisha alama 46 na michezo 22 akishikiria bado nafasi ya pili nyuma ya Yanga Fc mwenye alama 56 kwenye kilele cha NBC PREMIER LEAGUE.

Aidha stori kubwa kwa mchezo wa leo ni goli la Nahodha wa Simba John Rafael Bokko ambaye amefunga goli lake la kwanza msimu huu.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI