MANCHESTER NA LIVERPOOL ZAGAWA VICHAPO

Manchester.


Timu ya Manchester United imetoa kichapo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya ligi ya Uingereza.

Nyota wa mchezo wa leo ni Cristiano Ronaldo aliyepachika magoli 3 huku akifikisha jumla ya magoli 808 kwenye Kalia yake ya uchezaji wa mpira.

Naye ,mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefikisha jumla ya magoli 94 ya kufunga ugenini akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester Wayne Rooney aliekuwa na jumla ya magoli 93.

Manchester anashika nafasi ya 5 akiwa nyuma ya Manchester City,Liverpool,Chelsea na Arsenal ikiwa imecheza jumla ya michezo 28.

Kwingineko,Liverpool wameichapa Brighton magoli mawili kwenye ligi ya EPL na kuendelea kuchuana kuelekea kunyakua ubingwa wa EPL dhidi ya Manchester City.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI