ALIKIBA NA SHILOLE SASA NI DAMU DAMU

Dar es salaam.



Wasanii Alikiba na Shilole wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kipindi cha miezi minne ya msuguano.

Shilole ambaye ni msanii na mfanyabiashara alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya msanii mwenzake Alikiba kudai Shilole kuhudhuria kwenye shughuli yake bila kualikwa.Kauli hiyo ya Alikiba aliyoitoa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam ilimuibua Shilole alietokwa na maneno mazito aliyoyapost kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Shilole na Alikiba wamekubali kurudi kwenye ukaribu wao wa zamani ni baada ya mwana mama Shilole kusema yeye na Alikiba wamemaliza tofauti zao kijeshi.

Alikiba mpaka sasa hajatoa neno kuhusu kauli ya Shilole ingawa wawili ao walionekana kwenye tamasha la MwamiNtale mkoani Kigoma wakiimba na kukumbatiana jukwaani mapema mwezi February.

Maoni

HABARI KUU LEO

MBIVU NA MBICHI RIPOTI YA MAUAJI MTWARA MEZANI KWA RAIS SAMIA

Pep Guardiola says he will try to make his half-time team talks shorter after Manchester City were fined £2million for late kick-offs by the Premier League.

SABABU ZILIZOIONDOA GSM KWENYE MPIRA WA TANZANIA