Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2022

DIAMOND NA ALIKIBA MAMBO SAFI

Picha
Dar es salaam. Msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz akipiga stori kwenye kipindi cha "THE SWITCH" cha radio WASAFI FM inayorusha matangazo yake kutokea Mbezi beach ,Dar es salaam. Diamond Platinumz amesema hana wasiwasi wa kufanya kolabo na msanii Alikiba na hana ugomvi nae isipokuwa ni maneno ya mashabiki ,wanaowashindanisha kwenye mziki. Akipiga stori ,alijibu baadhi ya maswali ya watangazaji wa redio hiyo waliotaka kufahamu kama ana bifu na msanii mwenzake Alikiba,Diamond alikataa akidai kwamba kumshindanisha na wasanii wa ndani ni kuikosea tasnia ya mziki wa Bongo Fleva na watanzania pia.Diamond ambaye alifika kutambulisha EP yake ya "FOA" kwa mashabiki wake amejitambulisha kuwa sasa ni msanii namba 3 kwa Afrika. ila kuna mawazo ambayo watanzania tunatakiwa tuyafute ,ili wewe uonekane mkubwa lazima ugombane na mtu,Mimi sina noma halafu kila mtu namuheshimu kwa upande wake" Diamond Platinumz kwasasa anatoka na EP ya FOA yenye nyimbo kama Fresh📝📣so

KURASA ZA MAGAZETI LEO MACHI 14,2022

Picha
Dar es salaam Magazati ya leo yanasomeka hivi;-

LEMA NA ZITTO WATOFAUTIANA

Picha
Dar es salaam. Wanasiasa wawili maarufu nchini,Godbless Lema ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO ,Zitto Kabwe wamejikuta katika vita ya maneno kwa kutuhumiana. Godbless Lema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter ,amemfananisha kijana ambaye hakumtaja jina na mmoja wa mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Augustine Lyatonga Mrema,Mwenyekiti wa TLP Taifa.Lema amenukuliwa akiandika hivi;- "kuna kijana mmoja ana-behave na anataka aonekane kama mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP ,lakini yeye akiwa amechangamka zaidi" Baada ya andiko hilo ,naye Zitto Kabwe aliandika chini ya andiko hili kwa maneno yanayonukuliwa:- "Kijana huyohuyo,ndiye aliyekutoa wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa mwaka 2007 kwa kushirikiana na wadau wakiwemo viongozi wako kwasasa ndiyo watakuwekea mazingira mazuri ya siasa .Endelea wailing, sisi tunaweka mazingira mazuri ya kufanya siasa" Wafatiliaji wa Lema na wanaofatilia machapisho ya Lema walikuj

KURASA ZA MAGAZETI LEO MACHI 13,2022

Picha
 
MAKONDA AMUITA GSM TAPELI

Picha
Dodoma. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Shaka Hamdu,leo machi 12,2022 amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Katibu huyo alitaka kueleza kilichojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichokaa hivi karibuni. Shaka ameeleza kati ya mambo yaliyojadiliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM,Taifa ni pamoja na kuchunguza vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi hasa kuwaonea raia kwa kuwabambikizia kesi. Baada ya taarifa h iyo,aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda aliibuka na kuandika haya kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram "naunga hoja mkono ya kamati kuu ya kuchunguza mwenendo wa baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi ,wanalipaka tope jeshi la polisi kwa kuwalinda wafanyabiashara matapeli wanaodhulumu mali za watu.Naomba tuanze na Dar es salaam na mimi Paul Makonda nipo tayari kutoa ushirikiano. Haya ya Makonda yanajiri hivi karibuni baada ya kuwa na mgogoro wa nyumba yake iliyopo Masaki Dar es salaam inayothibitiwa na mfanyabiashara

MANCHESTER NA LIVERPOOL ZAGAWA VICHAPO

Picha
Manchester. Timu ya Manchester United imetoa kichapo cha magoli matatu kwa mawili dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye mechi ya ligi ya Uingereza. Nyota wa mchezo wa leo ni Cristiano Ronaldo aliyepachika magoli 3 huku akifikisha jumla ya magoli 808 kwenye Kalia yake ya uchezaji wa mpira. Naye ,mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane amefikisha jumla ya magoli 94 ya kufunga ugenini akivunja rekodi ya nyota wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester Wayne Rooney aliekuwa na jumla ya magoli 93. Manchester anashika nafasi ya 5 akiwa nyuma ya Manchester City,Liverpool,Chelsea na Arsenal ikiwa imecheza jumla ya michezo 28. Kwingineko,Liverpool wameichapa Brighton magoli mawili kwenye ligi ya EPL na kuendelea kuchuana kuelekea kunyakua ubingwa wa EPL dhidi ya Manchester City.

KAJALA AFUNGA KUMUOMBEA MONALISA

Picha
Dar es salaam. Frida Masanja au Kajala Masanja ;ni staa mkubwa wa Bongo Movies ambaye amemshukru MUNGU baada ya watanzania waliokuwa nchini Ukraine kufanikiwa kuondoka kutokana na vita akiwemo mtoto wa mwigizaji mwenzake ,Monalisa aitwaye Sonia. Kajala anasema kuwa,alifunga na kumuombea Sonia ambaye alikuwa masomoni nchini humo hili aweze kupita salama katika hali iliyotea Ukraine na kwasasa anamshukru MUNGU kwaajili ya Sonia kurudi na kuungana na familia yake akiwa salama.Sonia ni miongoni mwa watanzania waliofanikiwa kuondoka Ukraine wakiwa salama kupitia Urusi. Kajala Masanja akizungumza na Gazeti la IJUMAA ,anasema kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno alichokuwa anapitia Monalisa na yeye kama mzazi anajua machungu aliyoyapitia mwenzake.

MORRISON HANA CHAKE SIMBA

Picha
Dar es salaam. Akizungumza na mashabiki na wanachama wa Simba ,Rais wa heshima wa timu hiyo Mohamed Dewji kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ametolea ufafanuzi mambo mengi likiwepo suala la nidhamu ndani ya timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam. Mohammed Dewji  "Viongozi wetu wananidhamu kubwa ,tunataka kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu .Kama mchezaji atakuwa hana nidhamu basi tutaagana naye .Tunataka kujenga timu yenye nidhamu." Wakati haya yakijiri ni hivi karibuni mchezaji Bernard Morrison alionekana kuwa kwenye msuguano na viongozi wakuu wa Simba akiwepo mtendaji mkuu Barbara Gonzalez. Klabu ya Simba ililazimika kumfungia raia huyo wa Ghana kutocheza mechi na kufanya mazoezi na timu yao lakini baadaye mchezaji huyo alilazimika kuandika barua ya kuomba msamaha,klabu ya Simba ilikubali na kumrudisha kambini ingawa Morrison amekuwa na matukio ya kujirudia ya utovu wa nidhamu tangu aikimbie klabu ya Yanga . Kauli ya Mohammed huenda ikawa taya

ALIKIBA NA SHILOLE SASA NI DAMU DAMU

Picha
Dar es salaam. Wasanii Alikiba na Shilole wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kipindi cha miezi minne ya msuguano. Shilole ambaye ni msanii na mfanyabiashara alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya msanii mwenzake Alikiba kudai Shilole kuhudhuria kwenye shughuli yake bila kualikwa.Kauli hiyo ya Alikiba aliyoitoa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es salaam ilimuibua Shilole alietokwa na maneno mazito aliyoyapost kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Shilole na Alikiba wamekubali kurudi kwenye ukaribu wao wa zamani ni baada ya mwana mama Shilole kusema yeye na Alikiba wamemaliza tofauti zao kijeshi. Alikiba mpaka sasa hajatoa neno kuhusu kauli ya Shilole ingawa wawili ao walionekana kwenye tamasha la MwamiNtale mkoani Kigoma wakiimba na kukumbatiana jukwaani mapema mwezi February.

KURASA ZA MAGAZETI LEO MACHI 12,2022

Picha
Dar es salaam. Mambo vipi Tanzania. Magazeti ya leo yanasomeka hivi,tafadhali endelea kutembelea blog hii kila siku kupata vichwa vya magazeti ya siku husika.