LEMA NA ZITTO WATOFAUTIANA

Dar es salaam.


Wanasiasa wawili maarufu nchini,Godbless Lema ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa ACT WAZALENDO ,Zitto Kabwe wamejikuta katika vita ya maneno kwa kutuhumiana.

Godbless Lema kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter ,amemfananisha kijana ambaye hakumtaja jina na mmoja wa mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Augustine Lyatonga Mrema,Mwenyekiti wa TLP Taifa.Lema amenukuliwa akiandika hivi;-
"kuna kijana mmoja ana-behave na anataka aonekane kama mpinzani wa kweli huku kimsingi yeye ni kama Mrema wa TLP ,lakini yeye akiwa amechangamka zaidi"
Baada ya andiko hilo ,naye Zitto Kabwe aliandika chini ya andiko hili kwa maneno yanayonukuliwa:-
"Kijana huyohuyo,ndiye aliyekutoa wewe kwa Mrema ukaingia ulipo sasa mwaka 2007 kwa kushirikiana na wadau wakiwemo viongozi wako kwasasa ndiyo watakuwekea mazingira mazuri ya siasa .Endelea wailing, sisi tunaweka mazingira mazuri ya kufanya siasa"
Wafatiliaji wa Lema na wanaofatilia machapisho ya Lema walikuja juu kwa kugundua kwamba Lema alimlenga Zitto Kabwe ,jambo ambalo liliibua hisia mseto kwa wa wachangiaji.

Majibizano haya ya nguli wa siasa nchini yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini huku chama cha CHADEMA kikishindwa kupeleka wawakilishi.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI