MORRISON HANA CHAKE SIMBA

Dar es salaam.



Akizungumza na mashabiki na wanachama wa Simba ,Rais wa heshima wa timu hiyo Mohamed Dewji kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ametolea ufafanuzi mambo mengi likiwepo suala la nidhamu ndani ya timu hiyo ya mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam.

Mohammed Dewji 
"Viongozi wetu wananidhamu kubwa ,tunataka kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu .Kama mchezaji atakuwa hana nidhamu basi tutaagana naye .Tunataka kujenga timu yenye nidhamu."
Wakati haya yakijiri ni hivi karibuni mchezaji Bernard Morrison alionekana kuwa kwenye msuguano na viongozi wakuu wa Simba akiwepo mtendaji mkuu Barbara Gonzalez.

Klabu ya Simba ililazimika kumfungia raia huyo wa Ghana kutocheza mechi na kufanya mazoezi na timu yao lakini baadaye mchezaji huyo alilazimika kuandika barua ya kuomba msamaha,klabu ya Simba ilikubali na kumrudisha kambini ingawa Morrison amekuwa na matukio ya kujirudia ya utovu wa nidhamu tangu aikimbie klabu ya Yanga .
Kauli ya Mohammed huenda ikawa tayari inatoa ishara kwamba Bernard hatokuwa sehemu ya Simba kutokana na pia mkataba wake na Simba kuwa umebakiza miezi kadhaa.

Bernard Morrison alijiunga Simba akitokea Yanga ,tukio ambalo lilimuingiza katika mgogoro na Yanga mpaka kupelekana kwenye mahakama ya michezo CAS na Bernard Morrison alifanikiwa kuwaangusha Yanga.

Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI