Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2022

LIVERPOOL YATWAA UBINGWA WA CARABAO CUP

Picha
London. Timu ya majogoo wa Anfliend Liverpool  imetwaa ubingwa wa kombe la Carabao kwa jumla ya mikwaju ya Penati 11 na timu ya Chelsea imepoteza mkwaju wa golikipa Kepa Alzabaraga. Mechi hiyo iliyochezwa kwa jumla ya dakika 120 na kushuhudia ndani ya dakika 90,jumla ya magoli matatu yakikataliwa na VAR.

YANGA YAICHAPA KAGERA SUGAR 3

Picha
Dar es salaam. Timu ya wananchi Yanga imejiweka juu ya msimamo wa ligi ya NBC PREMIER LEAGUE kwa alama 42 mbele ya Simba na Azam. Yanga Sports Club wamejipatia magoli yao kupitia Fiston Mayele (30",52) na Saido Ntibazonkiza (65"). Yanga wanafikisha alama 42 tofauti na Simba wenye alama 31. Wafungaji bora ndani ya kikosi cha kocha Nabil ni Fiston Mayele mwenye magoli 9 , Saido Ntibazonkiza magoli 6 na Feisal Salim "fei Toto" mwenye magoli 4. Msimu uliopita mpaka ligi inaisha mfungaji wa Yanga alikuwa Deu Kaseke (6) na  Yacouba Sogne (6).

SIMBA YAKUBALI KUCHAPWA NA MBEYA CITY

Picha
Mbeya. Timu ya Simba sports club ya jiji Dar es salaam imekubali kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa Mbeya City ya jijini Mbeya.

HIZI NDIZO SABABU ZA SPIKA JOB NDUGAI KUJIUZULU

Picha
Dodoma. Aliyekuwa Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai amejitokeza na kutaja sababu za kuachana na uspika huo.

ZUCHU- Mwambieni (Official Lyrics)

Picha
Wimbo wa msanii Zuchu umetoka na ndio lyrics zake.

HISTORIA YA MPIGANIA UHURU AFRIKA DESMOND TUTTU(90)

Picha
Johannesburg. Habari ya kuhuzunisha ni ya kufuatia aliyekuwa Askofu wa muda mrefu wa jimbo la Gauteng ,Desmond Tuttu kufariki akiwa na umri wa miaka 90. Hii ndio historia yake mwanamajumui wa Afrika.

YANGA YAICHAPA BIASHARA 2-1 KWENYE LIGI YA NBC TANZANIA.

Picha
Dar es salaam. Timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kuichapa timu ya Biashara ,Mara jumla ya magoli mawili (2) kwa moja (1). Mpaka sasa Yanga wanaongoza ligi ya NBC PREMIER LEAGUE.

HOTUBA YA RAIS SAMIA MKOANI MARA

Picha
MUSOMA. Rais wa Tanzania Samia Suluhu leo amefanya ziara ya kikazi ya siku 3 mkoani Mara ,katika ziara hiyo Rais anategemea kufungua na kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo imesema taarifa ya mkuu wa mkoa huo Ally Happi.

SIMBA YAICHAPA ASEC 3 -1 MICHUANO YA SHIRIKISHO

Picha
Dar es salaam Timu ya ASEC MIMMOSA imekubali kipigo cha magoli 3 dhidi ya 1 mbele ya Simba Sports Club ya Tanzania kwenye michuano ya Shirikisho barani Afrika. _Tazama magoli yote.

MAMBO 10 USIYOFAHAMU KUHUSU VLADIMIR PUTIN WA URUSI

Picha
CRIMEA. Rais wa Urusi Vladimir Putin  huenda akawa kiongozi mbabe zaidi Duniani kutokana na hatua ya majeshi yake kuipiga nchi ya Ukraine. Putin ameamua kuipiga Ukraine kama hatua ya kuonyesha jeuri yake kuwa anaweza kuilinda Urusi dhidi ya maadui wa nchi hiyo ya Ulaya Mashariki.

KURASA ZA MAGAZETI LEO JUMAPILI 27/02/2022

Picha

BILIONEA ROMAN ABRAMOVICH AJIUZULU CHELSEA

Picha
London Mmiliki wa timu ya Chelsea ya London Kaskazini ,bilionea Roman Abramovich amejiuzulu kwenye wadhifa wake na kuamua kuyaacha majukumu yake kwa bodi ya wadhamini wa klabu hiyo. Roman anajiuzulu kufuatia shinikizo kutoka katika bunge la Uingereza kutokana na kitendo cha Urusi kuivamia kijeshi nchi ya Ukraine. Bilionea huyo hajaacha kabisa umiliki wa klabu hiyo bali ameacha majukumu ya kuonekana kwenye viunga vya London ambako ndio maskani ya timu hiyo. Roman Abramovich amekuwa mmiliki wa Chelsea tangu mwaka 2003 na anatajwa kuwa rafiki wa karibu na Rais Vladmir Putin wa Urusi.

MBIVU NA MBICHI RIPOTI YA MAUAJI MTWARA MEZANI KWA RAIS SAMIA

Picha
Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda kwaajili ya kuchunguza mauaji katika Mkoa wa Mtwara na wilaya ya Kilindi,Tanga. Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo February 25,2022 jiji Dar es salaam ,Waziri Mkuu ameipongeza kamati hiyo kwa kazi kubwa waliofanya na kwa umakini mkubwa . Waziri Mkuu amenukuliwa " taarifa hii imeeleza kila kitu bayana kabisa na haya ndio matarajio ya serikali yetu kwamba mtumishi yeyote ndani ya serikali lazima awajibike kwa weledi ,uaminifu,na uadilifu mkubwa kwa kufanya shughuli hiyo shughuli za kuwatumikia wananchi zitakwenda vizuri sana". Akizungumza PM amesema taarifa ya kamati hiyo ataiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alitoa maagizo ya uchunguzi wa vifo vya watu mkoani Mtwara na Wilaya ya Kilindi,Tanga. Waziri Mkuu akinukuliwa amesema "

MATUKIO KWA PICHA RAIS SAMIA AKIWA DUBAI

Picha
Dubai. Matukio kwa njia ya picha Leo ni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufungua maenyesho yajulikanayo kama EXPO 2020 DUBAI. Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwakaribisha washiriki nchi 197

RAIS WA UKRAINE AKATAA KUIKIMBIA NCHI YAKE

Picha
Kiev. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine. Rais huyo amesema " mapambano yamefika,nahitaji risasi ,sio msaada wa kuondoka" Marekani na washirika wa Ukraine walikuwa tayari kumpa msaada Rais Zelensky kuondoka nchini mwake. Rais huyo ambaye amewahi kuwa mwigizaji wa majukwaani amekuwa Rais wa Ukraine tangu 2019.

KURASA ZA MAGAZETI JUMAMOSI YA 26/02/2022

Picha

ATHARI ZA VITA YA URUSI NA UKRAINE KWENYE MICHEZO

Picha
Dar es salaam. Vita ya Urusi na Ukraine ilioanza tarehe 23/02/2022 imezua sintofahamu kubwa duniani ambapo nchi nyingi zimeonyesha kutofurahishwa na hatua ya majeshi ya Urusi kuivamia na kuipiga Ukraine. Vita hii ambayo dunia inashuhudia haijaacha athari kwingine hata kwenye michezo athari zipo nyingi kama ifuatavyo:- Fainali za Uefa zabadilishwa: Fainali ya Uefa iliyotarajiwa kuchezwa 28 Mei kwenye uwanja wa St Petersburg imeamishiwa nchini Ufaransa kwenye uwanja wa     The stade de France uliopo mjini Paris. Manchester United imetangaza kuvunja mkataba wa udhamini na shirika la ndege la Urusi yaani     AEROFLOT ni baada ya majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine. Timu za Serie A kukaa kimya dakika 5: Ligi ya mpira wa miguu ya Italia yaani Serie A itashuhudia kuanzia leo timu za Milan na Udinese zikikaa kimya kwa dakika 5 kama ishara ya kutaka amani ya UKRAINE. BUNDESILIGA yaweka mabango uwanjani: Usiku wa leo utashuhudia vilabu vya Stuttgart na Hoffenheim vikiingia uwanjani na mabango ya