MBIVU NA MBICHI RIPOTI YA MAUAJI MTWARA MEZANI KWA RAIS SAMIA

Dodoma.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya kamati maalum aliyoiunda kwaajili ya kuchunguza mauaji katika Mkoa wa Mtwara na wilaya ya Kilindi,Tanga.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo February 25,2022 jiji Dar es salaam ,Waziri Mkuu ameipongeza kamati hiyo kwa kazi kubwa waliofanya na kwa umakini mkubwa .

Waziri Mkuu amenukuliwa "
taarifa hii imeeleza kila kitu bayana kabisa na haya ndio matarajio ya serikali yetu kwamba mtumishi yeyote ndani ya serikali lazima awajibike kwa weledi ,uaminifu,na uadilifu mkubwa kwa kufanya shughuli hiyo shughuli za kuwatumikia wananchi zitakwenda vizuri sana".



Akizungumza PM amesema taarifa ya kamati hiyo ataiwasilisha kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alitoa maagizo ya uchunguzi wa vifo vya watu mkoani Mtwara na Wilaya ya Kilindi,Tanga.

Waziri Mkuu akinukuliwa amesema "
Rais Samia anahitaji kuona matokeo tena matokeo yasiyomuonea mtu yeyote lakini matokeo yatakayomuwajibisha yeyote ambaye atagundulika kuhusika kutaka kuleta tafrani ndani ya nchi yetu".


Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI