ATHARI ZA VITA YA URUSI NA UKRAINE KWENYE MICHEZO

Dar es salaam.



Vita ya Urusi na Ukraine ilioanza tarehe 23/02/2022 imezua sintofahamu kubwa duniani ambapo nchi nyingi zimeonyesha kutofurahishwa na hatua ya majeshi ya Urusi kuivamia na kuipiga Ukraine.

Vita hii ambayo dunia inashuhudia haijaacha athari kwingine hata kwenye michezo athari zipo nyingi kama ifuatavyo:-

Fainali za Uefa zabadilishwa:Fainali ya Uefa iliyotarajiwa kuchezwa 28 Mei kwenye uwanja wa St Petersburg imeamishiwa nchini Ufaransa kwenye uwanja wa


   The stade de France uliopo mjini Paris.

Manchester United imetangaza kuvunja mkataba wa udhamini na shirika la ndege la Urusi yaani 


  AEROFLOT ni baada ya majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine.

Timu za Serie A kukaa kimya dakika 5:Ligi ya mpira wa miguu ya Italia yaani Serie A itashuhudia kuanzia leo timu za Milan na Udinese zikikaa kimya kwa dakika 5 kama ishara ya kutaka amani ya UKRAINE.









BUNDESILIGA yaweka mabango uwanjani:Usiku wa leo utashuhudia vilabu vya Stuttgart na Hoffenheim vikiingia uwanjani na mabango ya kuamasisha amani ya Ukraine ilejee baada ya majeshi ya Urusi kuivamia nchi hiyo.




Maoni

HABARI KUU LEO

GUARDIOLA AWAPIGA DONGO LIVERPOOL

YANGA NA ARSENAL ZAGAWA DOZI