DIVA ATANGAZA NDOA YAKE RASMI

Dar es salaam.

Mtangazaji wa kipindi cha LaviDavi kinachoruka kupitia radio ya WASAFI ya jijini Dar es salaam DivatheeBawse ametangaza rasmi ndoa yake.



Kupitia insta story staa huyo aliandika yafuatayo "mume wangu ,halali yangu kabisa @sheikh_abdulrazak_salum .Asante kwa kunioa na kunifanya kuwa mkeo halali kabisa__jamani nakupendaaaaaa sana mume wangu_can't wait for our Nikkah celebration Abdul wangu".

Ujumbe wa Diva ulijiri kwenye siku ya Valentine wakati siku hio ikitekwa na tukio la kampuni ya WASAFI kuandaa tukio lilipewa jina la MAHABA.



Divatheebawse amejipatia umaarufu mkubwa kupitia Clouds Fm na Wasafi Fm kwa vipindi tofauti tofauti vya mapenzi.



Mme wa Diva huyu hapa aitwaye Abdulrazak Salum


Maoni

HABARI KUU LEO

MBIVU NA MBICHI RIPOTI YA MAUAJI MTWARA MEZANI KWA RAIS SAMIA

Pep Guardiola says he will try to make his half-time team talks shorter after Manchester City were fined £2million for late kick-offs by the Premier League.

SABABU ZILIZOIONDOA GSM KWENYE MPIRA WA TANZANIA