Machapisho

JINSI YA KUONGEZA KIPATO

Picha
Uchumi. Dunia ya leo ya mapinduzi ya nne ya viwanda ni tofauti na Dunia ya enzi za Ujima ambapo binadamu alitegemea kutembea kutafuta mahitaji yake kama matunda,mizizi na nyama kwa kuokota. Kwenye Dunia ya leo inakuhitaji kuwekeza katika maarifa zaidi ,ambapo utafungua akili na kuona fursa na kuziendea na pia utahitaji kuanza kuwekeza .Uwekezaji una maana pana ingawa watu wengi hufahamu uwekezaji ni pesa pekee ambalo sio kweli.Uwekezaji ni sawa na kumwambia Fundi wa nguo ashone suti,fundi akiambiwa suti yeye hupata picha kamili kwenye akili yake kwahiyo fundi mpaka anatoa hiyo nguo basi tunasema nguo inayoonekana ni picha ya kilichomo ndani ya fundi. Uwekezaji ni mawazo kwanza na ndio pesa hufuatia. Namna ya kuongeza kipato

MANCHESTER CITY YAICHAPA 4 MAN UNITED

Picha
Manchester Vilabu hasimu vya mji mmoja leo vimekutana kwa mchezo wa ligi ya EPL.Manchester United wakisafiri mpaka viunga vya Etihad wamekutana na kichapo cha magoli manne kwa moja (4-1). Manchester City imejipatia karamu ya magoli kupitia Kelvin De bryune aliekwamisha magoli mawili (2) huku Mahrez nae akiingia kambani mara 2 na goli la mashetani wekundu likifungwa na Sancho "20. Kelvin De'bruyne amepiga mashuti yake pekee kwenye lango la United mara 6 huku Manchester United ikipiga jumla ya mashuti 5. De bruyne amepiga pekee mashuti yaliyolenga goli 4 dhidi ya 2 za Man united na ametengeneza nafasi 5 pekee dhidi ya 2 zilizotengenezwa na Manchester United nzima. Naye kocha wa Manchester City , Pep Guadiola  akuwa nyuma ni baada ya kusema hakuwahi kupata upinzani kama huo wa Manchester United leo kwenye kipindi chote cha kazi ya ukocha miaka 15 iliopita.

CHELSEA YAICHAPA 4 BURNLEY

Picha
London Burnley wakisafiri kwenda mjini London kuifata timu ya Chelsea Fc wamepokea kichapo cha magoli manne bila majibu. Chelsea chini ya mkufunzi , Tomas Tuchel imejipatia magoli kupitia kwa     Reece James 47',Harvertz 52' 55" na Christian Pulsic 69". Urejeo wa James umeirejesha Chelsea kwenye makali yake maana winga huyo amefunga na kusaidia goli lingine. Chelsea wanasalia nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester city. Kwingineko, Liverpool imeichapa Westham goli moja kupitia kwa Sadio Mane. Matokeo mengine     Norwich 1-3 Brentford    Newcastle 2-1Brighton    Wolves 0-2 Crystal palace    Aston villa 4-0 Southampton

DRAKE ANUNUA NYUMBA YA NDOTO YAKE

Picha
Los Angeles. Rappa Drake wa nchini Marekani amenunua nyumba yenye thamani ya dola za marekani milioni 85 sawa na bilioni 187 za shilingi ya Tanzania. Nyumba hiyo iliyopo eneo la Beverly Hills mjini Los Angels nchini Marekani ina ukubwa wa futi za mraba 25,000 . Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala 10,bafu za kuogea 22,gereji za magari 11,gym na viwanja vya mchezo wa tenisi.